Terry azidishiwa kibano UEFA
LONDON,
England
NOHODHA
wa timu ya ya soka ya Chelsea, John Terry, ameongezewa adhabu ya kukosa mechi
mbili za ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu
dhidi ya Barcelona, katika mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo.
Terry alioneshwa
kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumpiga kwa goti beki wa Barcelona, Alexis
Sanchez, wakati wa mechi ya pili ya marudiano, aliikosa mechi ya fainali ya
michuano hiyo iliyowapa kombe.
UEFA iliamua
kumfungia Terry mwechi tatu kwa mchezo mbaya dhidi ya mchezaji huyo, ingawa
mechi ya fainali iliyochezwa Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich itahesabiwa.
Kwa
hiyo, atazikosa mechi za kuwania kombe la Ulaya kwa klabu dhidi ya Atletico
Madrid, na mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ya ligi ya Ulaya.
"Bodi
ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) , limemsimamisha mchezaji wa Chelsea FC, John Terry mechbi tatu
za michuano hiyo," taarifa ilisomeka. "Kwa mchezaji huyo hakushiriki
mechi ya fainali dhidi ya Bayern Munich Mei 19, tayari ametumikia mechi moja.
"Mechi
mbili zilizobaki, atatumikia michuano ya klabu ya UEFA ambayo timu yake
itashiriki. Rufani inawezekana ikawasilishwa siku tatu tangu itangazwe iwe na
sababu maalum."
No comments