Rodgers apata ulaji Liverpool, arithi mikoba ya Kenny Dalglish
LIVERPOOL, England
KOCHA mpya wa timu ya Liverpool, Brendan Rodgers,
amesema ataanza mipango yake kwa kuijenga timu hiyo kwa ajili ya ligi ya
England, baada ya kukabidhiwa mikoba na kuwa kocha wa 18 kuifundisha timu hiyo.
Rodgers alitakiwa kuwasili Anfield jana,
baada ya makubalino na klabu yake ya zamani ya Swansea City, na muda mfupi
akaweka wazi mipaango yake hiyo.
"Hii ni kazi ya muda mrefu,"
alisema Rodgers. "Ninataka kusimamia taratibu za klabu, soka la
kushambulia na nidhamu.
"Inawezekana ikawa miaka 20
imepita tangu itwae ubingwa, tuwa wazi, hatutakuwa tayari sasa, lakini, mipango
inaanza leo."
Rodgers alisema amefurahi kuwa kocha
wa pili kutoka Ireland kuifundisha Liverpool, na kwamba, awali aligoma kuhojiwa, lakini
baada ya kuthibitishwa, ikajulikana kuwa, ni chaguo la kwanza Liverpool ,
ambapo haikuwa vigumu kwake, kuondoka Swansea.
"Siku nyingi nilikuwa nikisema,
nitaondoka Swansea na kutua klabu kubwa, lakini nilipenda kuwa namba moja,"
alisema. "Kwa wakati huu, nilikuwa sehemu ya wanaobaki Swansea, lakini
iliibuka tena na kuwa wa kwanza kutaikiwa.
"Mara nilipojua nimekuwa wa
kwanza kusakwa, nilijiuzulu na ilikuwa rahisi."
Rodgers mwenye miaka 39, lakini
alikanusha taarifa za kwamba, ametwaa kiti hicho akiwa na uzoefu mdogo, lakini
alitoa mfano kwa mtangulizi wake, Kenny Dalglish, aliyeanza kufuundisha akiwa
kocha mchezaji na kufanikiwa kutwaa ubingwa na Kombe la FA.
"Mimi ni kijana kwa umri, lakini
nina uzoefu wa mechi nyingi," alisema. "Soka ni soka, wanataka kujifunza na wanataka kuelimika, na
ndicho nilichokifanya katika majukumu yangu."
Mwenyekiti wa Liverpool , Tom
Werner, aliyemtangaza Rodgers kwa
waandishi wa habari, ualielezea uzoefu wake uliowafanya wampe mkataba kocha
huyo wa zamani wa Reading.
No comments