Lyato aweka wazi kanuni za uchaguzi Yanga
Lyato (katikati) |
MWENYEKITI wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF), Deogratias Lyatto, ameweka wazi kuhusu usimamizi wa uchaguzi wa viongozi
wa klabu ya Yanga kujaza nafasi
zilizowazi za wajumbe wa kuchaguliwa wa kamati ya utendaji waliojiuzulu na
nafasi iliyo wazi kutokana na kifo cha mjumbe wa kamati hiyo.
Lyatto alisema, mchakato wa uchaguzi ambao umeanza,
utafanyika kwa kuzingatia kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF na kamati ya
uchaguzi ya Yanga itatekeleza wajibu na majukumu yake kwa mujibu wa katiba yake
ibara ya 45 mstari wa [1] na [2].
Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF,
idadi ya wajumbe wa kamati ya uchaguzi ni kati ya wajumbe watano5 hadi saba 7.
Lyato alisema kamati ya uchaguzi ya Yanga inayo wajumbe
watano, hata baada ya mjumbe mmoja kujiuzulu ili kukidhi matakwa ya kanuni za
uchaguzi za wanachama wa TFF ibara ya 3 mstari wa 2 na nafasi ya uongozi
aliyonayo TFF.
Alisema TFF inaamini kuwa, wajumbe wa kamati ya uchaguzi
ya Yanga watatekeleza wajibu na majukumu yao ya kikatiba na kikanuni
kuhakikisha kwamba, Yanga inajaza nafasi za viongozi zilizowazi katika mkutano
mkuu wa uchaguzi kwa kipindi kilichobaki cha mamlaka ya kamati ya utendaji
ibara ya 29 ya katiba ya Yanga, utakaofanyika Juni 15, 2012.
Mwenyekiti huyo, alisema kamati ya uchaguzi ya TFF
itatimiza wajibu na majukumu yake ya kusimamia kamati ya uchaguzi ya Yanga kwa
mujibu wa kanuni za uchaguzi na matakwa ya katiba ya YANGA, TFF na FIFA
yanazingatiwa.
No comments