Simba kumekucha Chang’ombe
![]() |
Simba |
MABINGWA wa soka
Tanzania Bara, Simba SC, leo wanatarajia kuanza rasmi mazoezi yake katika
Uwanja wa Sigara Chang’ombe jijini Dar es Salaam, wakiwa wamekamilika.
Kikosi hicho
kinatarajia kukamilika leo baada ya
wachezaji waliopewa likizo baada ya kuzitumikia timu zao za taifa, kuwasili
katika kikosi hicho.
Wachezaji wanaotarajiwa
kuanza mazoezi leo ni nahodha Juma Kaseja, Mwinyi Kazimoto, Amir Maftah, Nassor
Said, Haruna Moshi ‘Boban’ na Juma Nyosso waliokuwa katika kikosi cha Taifa
Stars.
Kwa upande wa
wachezaji waliosajiliwa msimu huu ni
Kanu Mbiyavanga kutoka DR Congo, Salum Kinje aliyetokea AFC Leopard ya Kenya, beki
Masombo Lino kutoka DC Motema Pembe ya DRC na kiungo Mussa Mudde kutoka
Sofapaka.
Wachezaji ambao
wamemaliza mkataba wao ni Ally Mustafa, Derick Walulya, Gervais Kago na Juma
Jabu, huku Rajabu Isihaka, Salum
Machaku, Haruna Shamte na Shija Mkina wakitolewa kwa mkopo.
Kikosi hicho
kitaanza kunolewa na Kocha Milovan Cirkovic baada ya kuwasili nchini akitokea
kwao Serbia likizo.
Mashabiki wa timu
hiyo waliohudhuria mazoezi ya jana, walisikika wakisema kuwa, ‘mashine’ zao
zote zitaanza mazoezi leo, hivyo kocha atakuwa na kazi kubwa ya kuangalia
wachezaji atakaowatumia katika kombe la Kagame.
Mazoezi hayo ni
kwa ajili ya maandalizi ya kombe la Kagame ambalo linatarajiwa kuanza Julai 14,
mwaka huu. Yanga ni mabingwa watetezi wa Kombe hilo.
Cirkovic, leo ataanza
rasmi kuinoa timu hiyo huku ikiwa imejaa nyota wake wote wapya na wa zamani
ambao walipewa likizo baada ya kuitumikia timu ya taifa.
No comments