Beckham aikosa michuano ya Olimpiki
![]() |
David Beckham |
LONDON, England
NDOTO za nyota wa zamani wa soka
nchini Uingereza, David Beckham, za kucheza michuano
ya Olimpiki mwaka huu, zimepotea, baada ya mchezaji huyo kuachwa kwenye kikosi
kitakachocheza michuano hiyo itakayofanyika jijini London.
Kocha Stuart Pearce, amemwacha
kiungo huyo wa Los Angeles Galaxy, katika kikosi chake kitakachocheza michuano
itakayoshirikisha timu 16, alikataa kumpa nafasi mchezaji huyo mwenye miaka 37,
katika idadi ya wachezaji watatu waliozidi miaka 23.
"Kila mmoja anajua jinsi
nilivyokuwa nikiichezea timu yangu, kwa hiyo wangenijumuisha kama kunienzi
katika kikosi cha GB," Beckham alisema katika taarifa yake iliyotolewa na
mwakilishi wake.
"Kwa kawaida, imenikatisha
tama, lakini haitakuwa na mashabiki wengi kama ambavyo ningekuwemo mimi na
ninawapenda, nina matumaini watatwaa medali ya dhahabu."
Beckham alikuwa sambamba na
Sebastian Coe kushawishi Kamati ya Olimpiki Duniani kuipeleka michuano hiyo
jijini London, ikiwa ni mara ya tatu kuandaa tangu mwaka 2005.
No comments