Balotelli amzadiwa mabao mama mlezi
![]() |
Balotelli |
WARSAW, Poland
MARIO
Balotelli, amesema kiwango alichokionesha na kuiwezesha timu yake ya Italia
kushinda mabao 2-1, dhidi ya Ujerumani katika hatua ya nusu fainali ya mataifa
ya Ulaya, ni usiku bora katika maisha.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 21,
anayeichezea timu ya Manchester City, alifunga mabao mawili katika kipindi cha
kwanza na kuiwezesha Italia kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, mabao hayo ametoa
zawadi kwa mama yake mlezi, Silvia.
"Balotelli alifanya kila awezalo
kwa England, lakini alipata zawadi yake dhidi ya Ujerumani. Kiwango chake
kilikuwa cha hali ya juu. Kilikuwa cha juu, nguvu na kufanikiwa kupata mabao. Aliongeza
kila kitu tulichokitaka kuongezwa kwenye mchezo. Kilikuwa kiwango kizuri."
Azzurri, sasa itaumana na Hispania
katika mechi ya fainali ya michuano hiyo.
"Ulikuwa usiku wenye furaha
katika maisha yangu ninaamini Jumapili utakuwa zaidi," alisema Balotelli.
Balotelli, aliiangailia familia yake
akiwakumbuatia. "Mwisho wa mchezo, nilirejea kwa mama, kwamba ilikuwa wakati mzuri," aliongeza.
"INilimwambia mama kuwa, mabao
niliyofunga ni wa ajili yako. Nilikuwa nikiisubiri siku kama hii, hasa kwa
mama yangu si kijana na hawezi kusafiri mbali, kwa hiyo ninatakiwa kumfurahisha.
Baba atahudhuria mechi ya fainali."
Balotelli, kwa mabao hayo mawili
aliyofunga, yamemwezesha kuwa miongoni mwa wachezaji wanaoongoza kwa kufunga
mabao mengi kwenye michuano hiyo, akiwa amekwamisha wavuni mabao matatu. "Nitajaribu
kufunga ili nitwae kiatu cha dhahabu," alisema.
Alishangilia bao la pili kwa mtindo
wa aina yake, kwa kuvua fulana na kusimama kimya. "Sikuchukia kwa sababu
nilioneshwa kadi ya njano, lakini waliona ukakamavu wangu," alitania.
Balotelli, ambaye alipumzisha
kipindi cha pili, alimaliza utata kuwa, atakuwemo katika kikosi kitakachocheza
kesho mechi ya fainali .
No comments