Nasri awangukia mashabiki Ufaransa
![]() |
Samir Nasri |
PARIS, Ufaransa
KIUNGO wa timu ya taifa ya Ufaransa,
Samir Nasri, amewaomba msamaha mashabiki wake kwa kumtolea maneno machafu
mwandishi wa habari baada ya mechi ya robo fainali dhidi ya Hispania.
Ufaransa katika mechi hiyo ilitolewa
kwa kuchapwa mabao 2-0 na kuanga michuano hiyo ya mataifa ya Ulaya mwaka huu
inayofanyika kwenye nchi za Ukraine na Poland.
Nasri alimtupia maneno mwandishi wa
habari akilalamika kuhusu tabia ya vyombo vya habari.
"Mashabiki wangu wakiwemo
watoto mnatakiwa kujua kuwa nilitumia lugha ambayo itakuwa imewashtusha," Nasri aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.
"Ninaipenda timu ya taifa ya
Ufaransa, soka na ninawaheshimu sana mashabiki."
Nasri, anayeichezea klabu ya
Manchester City, hakuomba msamaha kwa mwandishi, aliongeza: "Ni suala
binafsi kati ya mwanadishi na mimi. Nitaelezea vizuri siku ikifika."
Kocha wa Ufaransa, Laurent Blanc,
alisema tabia ya Nasri, ilionekana mbaya kwa mwenyewe na timu ya taifa.
"Inasikitisha, lakini ni tatizo
kati ya Samir na vyombo vya habari," Blanc aliiambia televisheni ya
Ufaransa.
Shirikisho la Soka Ufaransa,
linajiandaa kukutana na na Nasri wiki ijayo kusikia madai hayo.
Nasri alikuwa katika mechi hiyo
waliyofungwa na Hispania, na kuingia kipindi cha pili.
Kufuatia msuguano ulioripotiwa
kwenye kambi ya Ufaransa, baada ya kuchapwa na Sweden katika mechi ya mwisho ya
kundi lao, na kutupwa nje ya michuano hiyo, ikiwemo kutolewa kwenye fainali za
kombe la Dunia mwaka 2010.
Nasri alitoa majibu kwa kuweka
kidole chake mdomoni katika mechi dhidi ya England iliyomaliza kwa sare ya bao
1-1, pia ikiaminika kuwa, alivilenga vyombo vya habari.
Blanc alisema: "Nilimweleza
nini alichokuwa amekusudia kuhusu hili, baada ya tukio la kwanza, lakini naona
hakupata ujumbe."
No comments