Juventus yamfuatilia Balotelli Euro 2012
![]() |
Balotelli |
ROMA, Italia
WAKURUGENZI wawili wa klabu ya Juventus,
Fabio Paratici na Beppe Marotta,
wamekwenda nchini Poland kufuatilia kiwango cha mshambuliaji wa timu ya taifa
ya Italia, Mario Balotelli.
Corriere dello limeandika kuwa, Juve inavutiwa na mshambuliaji huyo wa Manchester City,
na wakurugenzi wake wawili wamekwenda jijini Warsaw kuzungumza naye.
Wakala wa Balotelli, Mino
Raiola, ana hofu kama Juve watakuwa na
fedha za kuishawishi City kuwamchia mshambuliaji huyo.
Mkurugenzi wa Juve, Pavel Nedved, wakati
huo huo alisema: "Niliwasiliana na Zlatan Ibrahimovic kuhusu Balotelli. Aliniambia kuwa, Mario ni bora na
alicheza naye."
No comments