Header Ads

ad

Breaking News

Mashabiki City wananipenda- Balotelli


MANCHESTER, England MARIO Balotelli, hana mpango ya kurejea tena Italia baada ya kumalizika kwa fainali za mataifa ya Ulaya, hata kama watatwaa kombe ya ubingwa huo.

 Mshambuliaji huyo atarejea Manchester City ambako anasema kuwa, mashabki wanampenda.
Pamoja na Balotelli kuchangia kuitoa England katika michuano ya mataifa ya Ulaya hatua ya robo fainali wiki iliyopita. 

City iliilipa Inter Milan pauni milioni 22, kumsajili Balotelli mwaka 2010, lakini hivi sasa klabu za nchini Italia zinapanga foleni ya kutaka kumrudisha nyumbani kwao. 

Aliulizwa kama anataka kurejea kwao, Balotelli alisema: “Kurudi nyumbani sasa? Ninarudi Manchester.
“Mashabiki wa City, wakati wote wananitaka, hata kama ni waingereza, na nilisaidia kutolewa kwa timu yao ya taifa.” 

Baada ya kufunga mabao mawili katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani, Balotelli anajiandaa na mechi ngumu katika maisha yake ya fainali. 

Fainali ya leo dhidi ya Hispania, ni nafasi nyingine kwake kuthibitisha kwamba, atatawala vichwa vyote vya habari kwa msimu sahihi. 

Balotelli alisema: “Ni mwaka maalum kwangu.
“Tumetwaa ubingwa wa ligi na Manchester City msimu uliopita, kwa hiyo tuna msimu mzuri haitegemei na kutwaa ubingwa wa Ulaya. 

“Ndio, itakuwa kitu maalum kwangu, lakini kama hatutashinda, haitabadili kitu.”
Kocha wa timu ya taifa ya Italia, Cesare Prandelli, alimpongeza Kocha wa City, Roberto Mancini, kwa kumjenga Balotelli. 

Alisema: “Ana uwezo mkubwa. Ana kocha mzuri Mancini, aliyemsaidia kumkuza.
“Mario hivi sasa anataka kurejea katika kiwango cha juu kama ilivyokuwa dhidi ya Ujerumani Jumapili,” Miongoni mwa kikosi cha Hispania, Balotelli anacheza timu mmoja na David Silva.

No comments