Man City yamtega Van Persie kwa pauni 225,000
MABINGWA wa ligi kuu England, Manchester City, wanajiandaa kutuma ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Robin van Persie.
Gazeti la Daily Star, limeandika kuwa, City wamejipanga kumwagia mshahara wa pauni 225,000, kwa wiki ambao utamshawishi kuiacha Arsenal na kutua Etihad.Mshambuliaji huyo anaongoza kwa wachezaji wanaotakiwa na Kocha wa Man City, Roberto Mancini, ambapo wanaamini Van Persie hawezi kukataa ofa hiyo.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, ana nia ya kumbakiza Van Persie, lakini kwa pauni milioni 11 kwa mshahara wa mwaka, utamfanya Mholanzi huyo kukimbilia City.
Wakati wakihaha kusaka saini ya Van Persie, klabu hiyo inapigania kuhakikisha inambakiza David Silva anayetakiwa na mabingwa wa Hispania, Real Madrid.
Gazeti la Daily Sta, limeandika kuwa, Real imeweka wazi kutaka kumsajili Silva kutoka Manchester City kwa kitita cha pauni milioni 30.
No comments