ILALA YAENDELEA KUGAWA POINTI COPA
![]() |
Ofisa Habari TFF, Boniface Wambura |
Ilala imeendelea
kufanya vibaya kwenye michuano ya Copa Coca-Cola baada ya leo asubuhi (Juni 28
mwaka huu) kuchapwa mabao 4-0 na mabingwa watetezi Kigoma katika mchezo
uliochezwa Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam.
Mabao yote katika
mechi hiyo ya kundi A yalifungwa kipindi cha kwanza huku Ramadhan Salum akipiga
hat trick (mabao matatu). Alifunga mabao hayo dakika ya 13, 43 na 45. Bao la
pili kwa washindi lilifungwa dakika ya 19 na Athuman Rashid.
Wakati Kigoma
imeshinda mechi mbili kati ya tatu ilizocheza mpaka sasa katika kundi hilo,
Ilala imepoteza mechi zote tatu ilizocheza. Ilala imefungwa na Arusha, Kigoma
na Lindi wakati mechi yake inayofuata itakuwa Juni 30 mwaka huu dhidi ya Kusini
Pemba.
Nayo Kilimanjaro
imeendelea kufanya vizuri katika kundi lake la D baada ya leo asubuhi (Juni 28
mwaka huu) kuitandika Shinyanga mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume, Dar es Salaam.
Mabao ya Kilimanjaro
ambayo hadi sasa imeshinda mechi mbili na kutoka sare moja yalifungwa na Adam
Soba dakika ya 11 na 46 wakati la tatu lilifungwa dakika ya 81 na James Henry.
Katika mechi nyingine
zilizochezwa leo asubuhi (Juni 28 mwaka huu), Temeke na Mtwara zilitoka sare ya
bao 1-1 kwenye Uwanja wa Tamco mkoani Pwani. Ali Makalani alianza kuifungia
Temeke na baadaye Adam swaleh akaisawazishia Mtwara.
Uwanja wa Nyumbu
mkoani Pwani ulishuhudia Morogoro na Kaskazini Pemba zikitoka sare ya bao 1-0.
Amin Kassim aliifungia Kaskazini Pemba dakika ya 51, na Morogoro wakasawazisha
dakika ya 75 kupitia kwa Mutalemwa Katunzi katika mechi hiyo ya kundi B.
Mechi zitakazochezwa
leo jioni (Juni 28 mwaka huu) ni Lindi vs Arusha (Tanganyika Packers), Manyara
vs Mjini Magharibi (Nyumbu), Kinondoni vs Mbeya (Tamco) na Kusini Unguja vs
Pwani (Karume).
Kesho (Juni 29 mwaka
huu) ni mapumziko, na michuano hiyo itaendelea tena Juni 30 mwaka huu kwenye
viwanja vyote vinne.
No comments