EXCLUSIVE: KAPOMBE + JONAS + 50 MILIONI = IBRAHIM JEBA
Mauzauza kwenye soka la Bongo
yameendelea kujidhihirisha leo.
Wakati klabu ya Simba ikiwa imejihakikishia kukamilisha usajili wa kinda la Azam under 20, Ibrahimu Jeba ambaye leo hii asubuhi alionekana kwenye mazoezi ya gym ya Simba - maeneo ya Chang'ombe. Uongozi wa klabu ya Azam FC umesema Simba inajidanganya kuhusu kumsajili mchezaji huyo ambaye Azam walimpeleka Villa Squad kwa mkopo kwa kujifua zaidi msimu uliopita.
Akizungumza na www.shaffihdauda.com kutoka nchini Marekani meneja wa klabu ya Azam FC, Patrick Kahemele amesema mabingwa wa Tanzania bara wanafanya uhuni kwenye uhamisho wa mchezaji huyo ambaye bado ana mkataba na klabu hiyo inayomilikiwa na mfanyabiashara Salim Bakheresa.

"Simba wanafanya uhuni
katika hili kama ilivyo kawaida yao, Jeba ni mchezaji wetu halali na bado ana
mkataba na Azam.
Kumbukumbu sahihi nilizonazo ni kwamba Ibrahimu Jeba alisaini
mkataba wa kuichezea Azam kwa miaka miwili mwezi Desemba 2011 na akachukua kiasi
cha fedha kama ada ya usajili - kabla ya kuelekezwa kwamba akacheze Villa Squad
kwa mkopo ili apate nafasi ya kujifua then msimu huu arudi Azam FC.
Simba
wakaenda wakamrubuni asicheze Villa, na Jeba bado mdogo hivyo ikawa rahisi
kumrubuni, na Azam hatukutaka kufanya nao malumbano kwa sababu suala hilo
tayari tuna mkataba ambao umesajiliwa kabisa na TFF, ambao walishatuambia haki
zetu za msingi zitalindwa."
Kahemele alipoulizwa ikiwa Simba wanataka kulimaliza hilo suala itabidi walipe kiasi gani alijibu, "Kiukweli sie tulishatangaza mapema kwamba hakuna mchezaji yoyote ambaye ameachwa wala yupo sokoni kwa msimu ujao.

Hivyo kama Simba wanamtaka Ibrahimu
Jeba kihalali basi atawagharimu sana kwa kuwa sisi tunamuona Jeba akiwa na
thamani ya Shilingi millioni 50 na uwachanganye wachezaji wawili wa Simba Jonas
Mkude na Shomari Kapombe, then hapo tunaweza kuwafikiria kuwaachia Jeba
vinginevyo haitowezekana Jeba kuichezea klabu yao."
HIKI NDIO KIKOSI RASMI CHA AZAM KWA AJILI YA MSIMU UJAO.
Kikosi Kamili cha Azam FC msimu ujao ni kama ifuatavyo Magolikipa ni Mwadini Ally, Deo Munishi "Dida" Aishi Salum na Jackson Wandwi.
HIKI NDIO KIKOSI RASMI CHA AZAM KWA AJILI YA MSIMU UJAO.
Kikosi Kamili cha Azam FC msimu ujao ni kama ifuatavyo Magolikipa ni Mwadini Ally, Deo Munishi "Dida" Aishi Salum na Jackson Wandwi.
Mabeki wa Pembeni kulia ni Ibrahim Shikanda na Erasto Nyoni na kushoto ni Waziri Salum na Samih Haji Nuhu
Babeki wa kati ni Luckson Kakolaki, Said Moradi, Joseph Owino na Aggrey Morris.
Viongo ni Kipre Bolou, Abdulhalim Humud, Himid Mao, Salum Abubakar, Abdi Kassim Sadala, Ramadhani Selemani Chombo, Abdulghani Ghulam, Ibrahim Rajab Jeba, Jabir Aziz Stima, na Ibrahim Joel Mwaipopo.
Washambuliaji wa pembeni ni Kipre Tchetche, Mrisho Ngasa, Zahoro Pazi, Khamis Mcha, na George Odhiambo "Blackberry" Washambuliaji wa kati ni Gaudence Mwaikimba na mchezaji bora wa Azam FC John Raphael Bocco "Adebayor"
No comments