TWIGA STARS, BANYANA ZAINGIZA MIL 8/-
Mechi ya kirafiki ya kimataifa kati
ya Twiga Stars na Afrika Kusini (Banyana Banyana) iliyofanyika Mei 20 mwaka huu
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 8,012,000.
Mapato hayo yametokana na washabiki
6,418 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 1,000, sh.
5,000 na sh. 1,000. Washabiki 6,057 walikata tiketi z ash. 1,000.
Asilimia 18 ya mapato ambayo ni sh.
1,222,169 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama
kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 1,560,000), waamuzi (sh. 650,000), usafi na
ulinzi (sh. 1,000,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000),
Wachina- Beijing Construction (sh. 500,000) na umeme (sh. 300,000).
Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya
gharama za mechi ni sh. 475,966, asilimia 10 ya uwanja sh. 237,983, asilimia 5
ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 118,992 na asilimia 65 ya TFF
(sh. 1,546,890).
No comments