MBWANA SAMATA, ULIMWENGU WAJIUNGA STARS
Mbwana Samata |
Washambuliaji Mbwana Samata na
Thomas Ulimwengu wanaocheza mpira wa kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wamejiunga na kambi ya timu ya Taifa
(Taifa Stars) jana (Mei 21 mwaka huu).
Wachezaji hao ambao ndiyo pekee
kutoka nje walioitwa na Kocha Kim Poulsen kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe
la Dunia Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast itakayochezwa Juni 2 mwaka huu jijini
Abidjan waliwasili jana saa 1.30 usiku kwa ndege ya Kenya Airways.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager inaendelea na mazoezi jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya
Karume na Taifa itacheza mechi ya kirafiki Mei 26 mwaka huu dhidi ya Malawi.
Mechi hiyo itafanyika Uwanja wa Taifa, na Malawi itawasili nchini Mei 24 mwaka
huu.
Baadaye Malawi itakwenda Zanzibar
kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Zanzibar Heroes itakayofanyika Mei 28
mwaka huu kabla ya kuondoka Mei 30 mwaka huu kwenda Uganda ambapo Juni 2 mwaka
huu itcheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika.
No comments