SERIKALI YAAMURU KUTUMIKA KWA MAFUTA YA NDEGE KUTOKANA NAUHABA WA MAFUTA YA TAA NCHINI
NA MWANDISHI WETU
MAMLAKA ya Udhibiti wa
Nishati na Maji (EWURA), imesema kutokana na uhaba wa mafuta ya taa uliyojitokeza
nchini serikali ina mpango wa kuyatumia mafuta ya ndege kama mbadala wa mafuta
hayo.
Akizungumza na Fullshangweblog
jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Titus
Kaguo alisema waliamua kuchukua hatua hiyo baada ya wafanyabiashara kuacha
kuagiza mafuta hayo kwa muda mrefu sasa.
Alisema kitakachofanyika ni
kubadili matumizi mafuta hayo ya ndege kwa kuyashusha daraja ili yaweze
kutumika kama mafuta ya taa ambapo hayata kuwa na madhara kwa watumiaji.
“Wafanyabiashara hao
waliacha kuagiza mafuta kutokana na baadhi yao, ambao si waaminifu kukosa
nafasi ya uchakachuaji hivyo, kupunguza kasi ya uingizaji wa mafuta hayo”alisema
Kaguo
Kaguo alisema
wafanyabiashara hao walikuwa wakiingiza hadi lita milioni 30 kwa mwezi lakini
baada ya serikali kufanikiwa kubana mianya ya uchakachuaji kiwango cha uingizaji
kimechuka hadi lita milioni 10 kwa mwezi.
Aidha, alisema licha ya
mipango hiyo, bado Mamlaka hiyo
imefanya mawasiliano na kuiagiza Kampuni ya PIC kuagiza mafuta hayo katika
kipindi muafaka ili kuwaondolea kero watumiaji wa mafuta hayo.
Kwa upande mwingine Kaguo
alizungumzia juu ya magari yaliyokamatwa wakati yakisafirisha mafuta nchini
Burundi kuwa wanaopaswa kujibu maswali hayo ni Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).
Alitanabaisha kuwa mafuta
yote yanayosafirishwa nje ya nchi yanasimamiwa na TRA hivyo yanapotokea
matatizo wahusika wakwanza ni mamlaka hiyo.
Kaguo alisema hata hivyo,
TRA iliwaomba ushirikiano ambapo walikubali na kwenda kuchukuwa sampuli na
kuipeleka kwa mkemia mkuu ili kupata ufumbuzi.
No comments