CUF YAWATAKA WAFUASI WAKE NA WANANCHI ZANZIBAR KUWA WATULIVU, WAVUMILIVU NA KUTOA MAWAZO YAO BILA JAZBA
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na katibu Mkuu wa chama cha CUF Maalim Seif Sharif Hamad.
Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Chama
cha Wananchi(CUF) kimewataka wananchi kutulia na Serikali kufanya
uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha vurugu zilizotokea mwishoni mwa
wiki Mjini Zanzibar.
Taraifa
ya Chama hicho kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa
Uenezi na Mahusiano na Umma,Salim Bimani ilisema “Chama cha CUF kinatoa
wito kwa wananchi wote kuwa watulivu, wavumilivu na kuitumia fursa ya
kutoa mawazo yao bila jazba na kutowanyima wengine nafasi ya kuwasilisha
mawazo yao”
Taarifa
hiyo ilisema kwamba vitendo vya watu wachache kuchoma makanisa moto na
kuharibu mali za watu ni vya uvunjifu wa sheria na kinyume na utamaduni
wa Kizanzibari.
“Uchunguzi
wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria bila
uonevu wala upendeleo” Alisema Bimani katika taarifa yake hiyo ambayo
pia alisema kwamba ni lazima kwa wakati huu na kwa haraka iwezekanavyo,
Serikali izungumze na Mashekhe bila ya kuona muhali na kwa uwazi kabisa
ili kutafuta suluhu ya kudumu kwa faida ya nchi.
Chama
hicho kimesema kwamba pamoja na sababu au visingizio mbalimbali
vilivyotajwa kuwa chanzo cha hali hiyo, zikiwemo za hamasa za wananchi,
chuki binafsi, ukosefu wa hekima,matumizi ya nguvu za dola na hata
uchochezi wa makusudi wa wale wanaoonekana kutokupendelea maridhiano ya
kisiasa Zanzibar.
“Chama
cha Wananchi,CUF, kama sehemu muhimu ya Umma wa Watanzania,hakiwezi
kukaa kimya kutokana na mwelekeo mzima wa hali tete ya amani katika
nchi, ingawa ni dhahiri wapo baadhi ya watu wasioitakia mema Zanzibar
wakibainika kufurahia mazingira hayo,kwa maslahi binafsi na pia kutoa
kauli za kutatanisha za kisiasa” Alisema Bimani katika taarifa yake.
No comments