MAKOCHA COPA COCA COLA KUSHIRIKI SEMINA YA FIFA
![]() |
Angetile Osiah |
Makocha
35 wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kushiriki
semina ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa ajili ya
michuano ya vijana ya Copa Coca-Cola.
Semina
hiyo itafanyika kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam kuanzia Juni
4-9 mwaka huu chini ya mkufunzi kutoka FIFA, Ulric Mathiot. Makocha hao
wanatakiwa kuripoti Juni 3 mwaka huu kwenye ofisi za TFF.
Makocha
hao na mikoa yao kwenye mabano ni Englihard Livigha (Mtwara), Joseph
Sehaba (Dodoma), Ramadhan Ramadhan (Mjini Magharibi), Shaha Khamis
Rashid (Kaskazini Unguja), Salum Ali Haji (Kusini Unguja), Mohamed Ali
Khamis (Kaskazini Pemba), Mecky Maxime (Morogoro) na George Simon
(Kagera).
Haruni
Dudu (Iringa), Maka Mwalwisi (Mbeya), Amos Mewa (Rukwa), Athuman
Kilundumya (Tabora), Charles Mayaya (Shinyanga), Fulgence Novatus
(Mwanza), James George (Mara), Amani Kongoro (Kigoma), Mtoro Likere
(Ilala), Evarist Katomondo (Kinondoni), Shawal Bilanga (Temeke) na
Rashid Chama (Arusha).
Wengine
ni Francis Samatta (Ruvuma), Issac Gamba (Kilimanjaro), Aloyce Mayombo
(Pwani), Jomo Puccey (Lindi), Justine Kanemela (Singida), Charles Msengi
(Manyara), Mohamed Kampira (Tanga), Alfred Itael (Arusha), Nicholas
Achimpota (Dodoma), Leonard Jima (Ruvuma), Leonard Malongo (Mwanza),
Kesi Abdallah (Tanga), John Memba (Ilala) na Zuhura Kapama (Kigoma).
No comments