CHIPUKIZI 10 WAPITA MCHUJO ASPIRE
![]() |
Wambura |
Wachezaji
10 wamepita katika mchakato wa kusaka vipaji kwa chipukizi wenye umri
chini ya miaka 14 kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football
Dream ambao uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) uliofanyika kuanzia Mei 21-26 mwaka huu.
Watoto
zaidi ya 1,500 walishiriki katika mchakato huo uliokuwa chini ya
mng’amua vipaji (scout) Gisbert Xavier kutoka Hispania, na ulifanyika
katika vituo vya Morogoro, Bagamoyo mkoani Pwani, na Kawe, Makongo,
Magomeni, Tabata, Kitunda, Tandika, Ukonga na Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume kwa Dar es Salaam.
Kituo
cha Morogoro amechaguliwa Karim Hussein wa Shule ya Sekondari Nanenane,
kituo cha Magomeni ni Joseph Mushi wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere
wakati kituo cha Tabata ni Martin Tangazi.
Tandika
ni Ismail Ngakonda (Shule ya Sekondari Uwanja wa Ndege), Kitunda ni
Nicholas Lauteri (Shule ya Sekondari Ulongoni), Omari Mbwai (Shule ya
Sekondari Msongola) na Hamad Omari (Shule ya Sekondari Ulongoni).
Kituo
cha Ukonga ni James Msuva (Shule ya Sekondari Makongo) wakati Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume ni Adolf Mtasigwa (Shule ya Sekondari Loyola) na
Ally Hatibu (Shule ya Sekondari Kurasini).
Mng’amuzi
huyo wa vipaji anatarajia kufanya mchujo wa mwingine kabla ya chipukizi
hao kwenda Nairobi, Kenya kwenye mchujo wa mwisho baada ya kambi ya ya
siku nne kuanzia Juni 5-9 mwaka huu.
No comments