Header Ads

ad

Breaking News

DK SHEIN AONGOZA MAZISHI YA BRIGEDIA JENERALI ADAM MWAKANJUKI ZANZIBAR


Wanajeshi wa JWTZ  wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Adam Mwakanjuki mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Abeid Karume Zanzibar kutokea Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi
(Picha na Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar) 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein,akitia saini kitabu cha kumbukumbu cha  Marehemu
Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki,katika ukumbi wa zamani wa
Baraza la Wawakilishi Manazi mmoja Mjini Unguja leo,marehemu atazikwa
katika makaburi ya mwanakwerekwe Zanzibar.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa
wameubeba Mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam
Mwakanjuki,na kuingia katika viwanja vya ukumbi wa zamani wa Baraza la
Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja leo,ambapo Viongozi mbali mbali
na wananchi pamoja na ndugu na jamaa, watatoa salamu zao za mwisho kwa
mwili wa Marehemu. .[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein,akitoa salamu za mwisho kwa Marehemu Brigedia
Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki,katika ukumbi wa zamani wa Baraza la
Wawakilishi Manazi mmoja Mjini Unguja leo,marehemu atazikwa katika
makaburi ya mwanakwerekwe Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akimpa pole mjane wa Marehemu Brigedia Jejerali
mstaafu Ikupi Adam Mwakanjuki,wakati wa kutoa salamu za mwisho kwa
mwili wa marehemu,katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilshi
Mnazi mmoja Mjini Unguja leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akiwapa pole jamaa na ndugu wa Marehemu Brigedia
Jejerali mstaafu   Adam Mwakanjuki,wakati wa kutoa salamu za mwisho
kwa mwili wa marehemu,katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilshi
Mnazi mmoja Mjini Unguja leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Baadhi ya wananchi,Jamaa na ndugu wa Marehemu waliofika
kutoa salamu za mwisho kwa mwili wa marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu
Adam Mwakanjuki,katika viwanja vya  zamani  Baraza la wawakilishi
Mjini Unguja jana.[Picha na ramadhan Othman.Ikulu.]

No comments