Simba yazidi kujiimalisha kileleni
Simba imezidi kujiimalisha kileleni mwa Ligi KUu Bara baada ya kuifunga Mtibwa Sugar ya Morogoro bao 1-0, katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Bao hilo pekee lilifungwa na mshambuliaji Emmanuel Okwi dakika ya 35 baada ya kumuhadaa beki Salvatory Ntebe na kupiga shuti lililotinga moja kwa moja wavuni akimalizia pasi iliyopigwa na Uhuru Seleman.
Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 18 kutokana na michezo nane iliyocheza huku Azam ikibaki katika nafasi ya pili kwa pointi 14 na Mtibwa imebaki katika nafasi ya tatu kwa pointi 12.
Dakika ya 89, Mtibwa ilipata nafasi pekee na kushindwa kuitumia ambapo Hussein Javu aliyeingia badala ya Ally Mohamed kuchelewa kupiga mpaka Victor Costa alipokuja kuondosha hatari akiwa ndani ya eneo la hatari.
Sekunde chache kabla ya kumalizika kwa mchezo, Simba ilipata penalti, lakini mpira uliopigwa na Victor Costa ulipanguliwa na kipa Deogratius Munishi 'Dida', penalti hiyo i8litokana na Haruna Moshi 'Boban' kufanyiwa madhambi na Shaabn Nditi ndani ya eneo la hatari.

No comments