T-Moto kuzawadia nguo mashabiki wao
Baadhi ya wasanii wa Kundi jipya la Muziki wa Taarab, la Tanzania Moto modern Taarab (T-Moto), wakiwa katika Studio za Makunde Production Kinondoni jijini Dar es Salaam leo, wakati wakirekodi nyimbo zao mpya zitakazokamilisha albam yao ya kwanza ya Aliyeniumba Hajanikosea
KUNDI jipya la Taarab la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) linalotarajia kuzinduliwa Oktoba 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam, limezindua mavazi yake rasmi kwa ajili ya kuwazawadia mashabiki wake siku ya uzinduzi.
Mkurugenzi wa Kundi hilo, Amini Salmini, amesema kuwa wameamua kuandaa Tisheti kwa ajili ya wanaume na Vitop vya Kidada, zenye Nembo ya kundi hilo kwa ajili ya mashabiki wa kundi hilo, watakaojitokeza kushudia uzinduzi wao.
Amini amesema kuwa Ujio wa kundi hilo utakuwa ni tofauti na makundi mengine yaliyopita kutokana na kujiandaa vilivyo na kulifanya kundi hilo kuwa ni la kipekee katika utendaji kazi na kujali maslahi ya kila msanii wa kundi hilo.
Amini amesema ameweka magita matatu katika kundi hilo, ili kuweza kuongeza radha ya muziki na kuleta uotafauti baina ya nyimbo za kundi hilo na nyimbo za makundi mengine.
Kundi hilo limeingia Studio za Bakunde Production zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam jana kuanza kurekodi nyimbo zake mpya zilizokamilika ili kukamilikamisha albam.
Wasanii wa Kundi jipya la Muziki wa Taarab, la Tanzania Moto modern Taarab (T-Moto), Mosi Suleiman (kushoto) na Hassan Ally, wakiwa katika Studio za Makunde Production Kinondoni jijini Dar es Salaam jana, wakati wakirekodi nyimbo zao mpya zitakazokamilisha albam yao ya kwanza ya Aliyeniumba Hajanikosea. Foto: sufianimafoto
No comments