Simba yalazimisha sare Kagera
MABINGWA wa Ngao ya Jamii, Simba ya Dar es Salaam, leo imelazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Kagera Sugar, katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera.
Simba walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Patrick Mafisango dakika ya 35, lakini mashabiki walishuhudia Felix Sunzu akikosa penalti.
Kagera Sugar ikicheza mbele ya mashabiki wake kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Kaitaba, walisawazisha bao hilo dakika ya 75, kupitia kwa Hussein Sued.
Bao hilo lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na kuifanya Simba kuondoka mkoani Kagera na pointi moja. Pamoja na matokeo hayo, Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 14, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 11.

No comments