Header Ads

ad

Breaking News

Sengeti Boys, Azam FC vijana zatoka sare


Beki wa timu ya Azam FC ya vijana wenye miaka chini ya 17, Ramadhani Mbega (kulia), na mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana wenye miaka chini ya 17, wakaniwa mpira wakati wa mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, jana. Foto: Zuberi Mussa.


TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' na timu ya vijana chini ya ya Azam FC miaka 20 zimetoka sare ya bao 1-1 mchezo wa iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao ulichezwa katika uwanja wa Karume  ulikuwa maalumu kwa Serengeti Boys kujiandaa na michuano ya vijana ya Coca Cola itakayofanyika mwakani London, Uingereza.

Azam ilikuwa ya kwanza kuandika bao la ushindi dakika ya 13 kupitia kwa mchezaji wake Jeba Agrey .........

Bao hilo liliwazindua vijana wa Serengeti Boys na kucheza kwa ushindani na kusawazisha dakika ya 38 kupitian kwa mshambuliaji wake Kimwaga Joseph.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kucheza kwa bidii lakini hata hivyo mpaka mpira unamalizika timu zote zilishindwa kutambiana.


@@@@@@

No comments