Judo wakubali muziki ulikuwa mzito kwao Msumbiji
KATIBU Mkuu wa Chama cha Judo Tanzania (JATA), Kashinde Shabani amekiri wachezaji wake kukutana na vigogo wa mchezo huo katika mashindano ya Afrika yaliyomalizika Maputo, Msumbiji wiki iliyopita.
Katika mashindano hayo Tanzania iliambulia medali ya moja ya fedha kupitia mchezo wa Netiboli na kushika nafasi ya 15 katika mashindano hayo ambapo sambamba na mchezo huo pia Tanzania ili wakilishwa na michezo mingine ya Majahazi, Riadha, Michezo ya walemavu (PARALIMPIKI), Ngumi za ridhaa na Soka la wanawake.
Katibu mkuu huyo amesema, wachezaji wake walikutana na wachezaji wenye uwezo wa juu na waliopata maandalizi ya kutosha nje ya nchi yao hivyo kushindwa kufurukuta ingawa walipeleka wachezaji wenye uwezo mkubwa hapa nchini katika mchezo huo.
Amesema, kwa upande wao maandalizi yalikuwa ya muda mfupi kwani timu ilijiandaa muda wa mwezi mmoja hivyo si rahisi kuweza kutoa matokeao mazuri hata kama wachezaji wanauwezo kiasi gani.
No comments