Header Ads

ad

Breaking News

CHANETA, CHANEZA zajipanga Olimpiki London


VYAMA vya Netiboli Tanzania Bara (CHANETA) na Zanzibar (CHANEZA), vinaanza mchakato wa michuano ya Olimpiki kwa netiboli itakayofanyika mwakani London, Uingereza.

Taifa Queens tayari imefuzu moja kwa moja kushiriki michuano ya Olimpiki, baada ya kunyakua medali ya fedha katika michuano ya Mataifa ya Afrika iliyomalizika Maputo, Msumbiji wiki iliyopita.

Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi amesema wamevunja kambi ya timu hiyo ya taifa, ili kupisha wachezaji kupata mapumziko mafupi, wao waendelee na maandalizi ya Olimpiki yatakayofanyika mwakani.

Taifa Queens ndiyo pekee waliotwaa medali katika michuano ya mataifa ya Afrika, licha ya Tanzania kuwakilishwa na timu sita za michezo tofauti.

No comments