Header Ads

ad

Breaking News

Wazee wanaume watakiwa kuacha tabia ya kujifungia nyumbani

Na Mwandishi Wetu
IMEELEZWA kuwa wazee wanaume wanapofikia umri wa kustaafu wanakuwa wazito sana kutoka na kushirikiana na jamii, jambo ambalo linaathari kutokana na takwimu kuonesha wazee wanaume wanakufa haraka kuliko wazee wanawake kwa sababu wanapenda kujifungia.

Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Philemon Foundation, Rodgers Mbaga katika Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani Oktoba mosi, ambapo amewashauri wazee wanaume kuachana na tabia hiyo.

“Hili la wanaume wazee kutopenda kutoka na kujumuika na jamii limejitokeza hata leo sisi tumewaalika wazee wapatao 200, lakini cha kushangaza wengi wa wazee waliotoa udhuru wa kutoshiriki kwa sababu mbalimbali ni wanaume,” alisema Mbaga.

Mbaga amewapa changamoto wanaume kujenga utayari wa kutoka na kuchangamana na jamii kwani kufanya hivyo ndio nafasi pekee ya kukabilian na misongo ya mawazo inayotokana na changamoto za maisha.

“Wanaume wengi pengine wakitoka sana wanaenda baa kupata kinywaji pengine wanadhani inawasaidia kupoteza mawazo, lakini wanakosa fusa nyingine zaidi ya kukutana na wazee wenzake na kubadilishana mawazo,” alisema Mbaga.

Mbaga ameeleza kwamba taasisi ya Philemon Foundation imekuwa ikijishughulisha na kundi la wazee wenye kipato cha kati, kutokana na kuwa Serikali mara nyingi imekuwa ikijishughulisha na kundi la wazee masikini.

“Lakini kuna kundi la wazee ambao suala la kujimudu kimaisha haliwapi shida sana, lakini wanashida ya upweke, wamesahaulika kwa sababu kila mtu kwenye jamii anamini hawa wapo kwenye maisha ya kujiweza hivyo hawana shida,” alisema Mbaga.

Amelitaja kundi hiyo ambalo jamii imelisahau kuwa ni la wazee wastaafu wa taasisi mbalimbali za umma na binafsi, wazee wastaafu wa shughuli zao binafsi zikiwamo za wafanyabishara na wakulima.

“Wazee hawa wengi wanaishia nyumbani wanachanganyikiwa hawatoki kwenda kazini, kwenda kwengine kwa hiyo wanakosa kuwa sehemu ya jamii, wengi watoto wao wamesha jiweza wanajitega wanakuwa wapweke,” alisema Mbaga.

Amesema Philemon Foundation kwa kutambua kuwa wazee ni hazina, wameamu kuangalia ni jinsi gani ya kutumia hazina hii ya wazee ili waweze kutumika katika jamii kutoa ushauri, kutoa elimu pamoja na ujuzi mbalimbali.

Kwa upande wao baadhi ya wazee walioshiriki maadhimisho hayo wamelalamikia kitendo cha vijana kuwanyanyapaa wazee wastaafu wenye ujuzi pindi waitwapo kazini kufanya kazi za mikataba ya muda mfupi na kuwaona kama hawafai kuwapo kazini.

Pamoja na mambo mengine Taasisi ya Philemon Foundation imezindua Sinior Citizen Club, ambayo itahusika kwa karibu na wazee katika masula mbalimbali yakiwamo ya kubadilishana mawazo, kupeana fusa mbalimbali pamoja na kutoa elimu mbalimbali zitakazowasaidia.




No comments