Header Ads

ad

Breaking News

Rais Dkt.Mwinyi arejea Unguja kufuatia kifo cha kaka yake

Zanzibar

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewasili Unguja akitokea Pemba kufuatia kifo cha kaka yake, Rubani Abbas Ali Hassan Mwinyi, kilichotokea leo Septemba 25,2025, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Marehemu Rubani Abbas Ali Hassan Mwinyi atazikwa kesho Ijumaa, Septemba 26, 2025, nyumbani kwao Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja, mara baada ya Sala ya Ijumaa.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.




No comments