Jumaa ataka Kibaha Vijijini iwe Kanda Maalumu michezo
MTEULE nafasi ya Ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Hamoud Jumaa, amesema kuwa pamoja na shughuli za kimaendeleo pia sekta ya michezo Jimbo hilo kitakuwa Kanda Maalumu.
Jumaa alitoa kauli hiyo akizungumza na Mwandishi wa Habari mjini hapa, ambapo alisema hatua hiyo inakwenda kuhakikisha Mpira wa Miguu ngazi ya Wilaya inachezwa ngazi zote.
Alisema kuwa amefuatilia kwa karibu sekta ya mchezo huo akajionea kuwa Ligi nyingi zinazoanzishwa na wadau wa mchezo huo, hatua ambayo pamoja inalenga kuibua na kuendeleza vipaji lakini haizipatii vijana nafasi ya kupanda Ligi za juu.
"Nitakwenda kukutana na uongozi wa Chama Cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kibaha (KIBAFA) kuona ni namna gani wanvyoweza kuziangalia Kibaha Vijijini kama Kanda Maalumu ili iweze kucheza Ligi," alisema Jumaa.
Aliongeza kuwa anatambua Jimbo lake linaitika katika Wilaya ya Kibaha, na kwa mujibu wa taratibu zao huwezi kuwa na chama kinachosimamia mchezo huo, lakini atakutana na viongozi wa chama hicho kuona ni namna gani wanvyoweza kufanikisha hilo.
"Kule Dar es Salaam nakumbuka kuna wakati Temeke iliwahi kuwa Mkoa wa kisoka, japokuwa iko ndani ya Mkoa hatua iliyolenga kuongeza wigo wa mchezo huo kuchezwa kwa nafasi zaidi na vilabu vingi vishiriki," alisema Mgombea huyo.
Aliongeza kuwa "Na huku Kibaha Vijijini nitakutana na viongozi wanaohusika na masuala hayo ili moja kati ya hilo lifanyike, ipatikane Kanda Maalumu au Ligi hiyo ianziie Vitongoji, Vijiji kuja juu hatua itayoongeza hamasa ya mchezo huo," alisema Jumaa.
Alisema kwamba amekuwa akishuhudia Mashindano yanayoandaliwa na wadau ambayo yanakuwa na hamasa kubwa vipaji vingi vinaonekana lakini kutokana na kuishia hapa hapa Kibaha Vijijini haileti tija kwa vijana.
Alimalizia kwa kusema kwamba alishihudia ushindani mkubwa uliokuwelo kwenye Ligi ya Samia Super Cup iliyoandaliwa na Jumuia ya Vijana (UVCCM), ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa.
"Nishuhudia ilivyoanza kwani nilihudhuria mpaka siku ya fainali, ambayo niliyadhamini kwa lengo la kuhamasisha mchezo huo, nina kiu ya kuona vijana jimboni kwangu wanaopata fursa ya kucheza Ligi ngazi za juu badala ya kuishia Mashindano ya mitaani Maarufu Ndondo," alimalizia Jumaa.
No comments