Header Ads

ad

Breaking News

Wanachama wa CCM Lugoba wavunja makundi

Godbles Naibala

Na Omary Mngindo, Lugoba  

SIKU chache baada ya kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanachama wa chama hicho Kata ya Lugoba, Chalinze Bagamoyo Pwani wamevunja makundi. 

Kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu ya chama hicho katani hapa chini ya Kaimu Mwenyekiti Hussein Kilala na Katibu Mwenezi, Shirazi Bashiri, wana CCM hao kwa kauli moja wamesema kuwa zoezi hilo liliendeshwa kwa haki. 

Kikao hicho kilichomtambulisha rasmi Godbles Naibala, kupeperusha bendera ya chama hicho Udiwani katani hapo, ambapo kabla ya kushinda nafasi hiyo alikuwa Mwenyekiti wa CCM katani hapo. 

Zaina Christofa mmoja wa wanaCCM ambao kura hazikutosha alisema kuwa mchakato ulikuwa wa haki na kwamba yeye na watu wake waliyokuwa wanaomuunga mkono wameungana na mgombea Naibala. 

"Tumeshamaliza kura za maoni ndani ya chama, sasa wote ni wamoja tunakwenda na wagombea wetu Godbles Naibala, ubunge Ridhiwani Kikwete na Dkt. Samia Suluhu ndio mgombea wetu wa Urais," alisema Christopha. 

Ucheche Idd alisema kuwa yupo ndani ya chama hicho kwa miaka mingi, ameshiriki chaguzi za ndani kati ya hizo kuna ambazo kura hazikutosh nyingine zilitosha hivyo anaungana na wanaCCM wenzake kuwanadi wagombea wao. 

"Chama chetu wote ni wamoja, tunapoingia katika harakati za uchaguzi tunakuwa na makundi, lakini pindi mchakato unapokamilika tunavunja makundi hayo kisha tunarudi kuwa wamoja," Idd. 

John Francis "Bolizozo" alisema kuwa wanakwenda kuwapambania wagombea wote wanaotokea ndani ya chama hicho na si vinginevyo, na kwamba makundi yao yaliisha tokea Agosti 4 baada ya kura za maoni. 

Akizungumza na wanaCCM hao, Naibala aliwashukuru wanachama hao huku akieleza kuwa anawategemea katika kufanikisha safari hiyo, itayofanyika Novemba 29 mwaka huu. 

"Nawaomba kura za Rais Samia Suluhu na Mbunge wetu Ridhiwani Kikwete ziwe za kutosha ndipo zije zangu, kwani kwa kupata kura nyingi Mimi haitoleta picha nzuri, pigeni za kutosha kwa wagombea hao," alisema Naibala. 

Kaimu Mwenyekiti Kilala aliwashukuru Wajumbe hao kwa Umoja wao waliouoneaha katika kipindi chote, huku akiwaomba kila mmoja akapambane kuhakikisha kura za kutosha zinapatikana kwa wagombea wao.



No comments