Header Ads

ad

Breaking News

UCSAF yataja mafanikio yake, yageukia kujenga uchumi wa kidijitali

 

Mkuruegenzi Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi Peter Mwasalyanda akitoa wasilisho lake mbele ya wahariri na waandishi wa habari leo Jumatatu Mei 25,2025 jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi Peterv Mwasalyanda amesema  serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imedhamiria kujenga uchumi wa kidijitali, hivyo wamejikita kuhakikisha  wanafanikisha huduma ya mawasiliano kwa wananchi wote.

Akizungumza katika kikao kazi na wahariri na waandishi wa vyombo vya habari kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, leo Jumatatu Mei 25,2025 jijini Dar es Salaam, Mhandisi Mwasalyanda amesema mikakati ya UCSAF ni kuhakikisha watanzania bila kujali sehemu wanazoishi kama ni mjini au vijijini wanafurahia huduma za mawasiliano na kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali.

Mhandisi Mwasalyanda, ameelezea mafanikio ya UCSAF kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Dkt.Samia Suluhu Hassan, ya kufikisha huduma ya mawasiliano sehemu mbalimbali za nchi.

"Mawasiliano ni sawa na huduma nyingine muhimu kama maji, umeme, ndiyo maana tunatakakila mwananchi awe na mawasiliano ya uhakika, mkulima kule vijijini awe na mawasiliano ya masoko, mfano Soko la Kariakoo," amesema.

Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utafiti wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi Albert Richard, akizungumza katika kikao kazi


Ameongeza kuwa, Mfuko huo katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita chini Dkt.Samia, wanatekeleza miradi 15, ikiwemo ujenzi wa minara ambao ni mradi wa kimkakati, huku wakiendelea na ujenzi wa minara 758.

Mkurugenzi huyo amesema miradi inayotekelezwa na UCSAF imegawanyika katika sekta tatu ambazo ni Sekta ya Mawasiliano (Simu na TEHAMA), Sekta ya Utangazaji na Sekta ya Post, ambapo UCSAF imeingia mikataba kufikisha mawasiliano katika Kata 1,974 zenye vijiji 5,111, wakazi 29,153,440.Jumla ya minara 2,152 itajengwa.

Mhandisi Mwasalyanda amesema kuwa, Mei 2023, serikali kupitia UCSAF iliingia mikataba na watoa huduma kufikisha mawasiliano maeneo ya vijijini, ambapo kupitia mradi huo kata 713 zitanufaika kwa kujengwa minara 758, wilaya 127na mikoa 26 itanufaika.

Ameongeza kuwa, katika miradi hiyo, wananchi milioni 8.5 watafikiwa na huduma za uhakika za mawasiliano, ambapo ruzuku shilingi bilioni 126 zitatumika, na kwamba hadi Mei 23,2025, minara 533 kati ya 758 tayari imewekwa na inatoa huduma. Hiyo ni sawa na asilimian 70.32.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Celina Mwakabwale akizungumza wakati wa kikao kazi

"Minara 304 imeongezwa nguvu kutoka 2G kwenda 3G/4G kwa kutumia ruzuku ya shiling bilioni 5.51, na minara 304/304 imekamilika," amesema.

Mkurugenzi Mkuu huyo, mradi wa kufikisha huduma ya mawasiliano Zanzibar mkataba wake ulisainiwa Januari 20,2022, ulitelekezwa kwa ushirikiano na Zantel/Honoraambapo Shehia 38 zimenufaika, minara 42 ikijengwa kwa ruzuku ya shilingi bilioni 6.9.

Afisa Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma Ofisi ya Msajili wa Hazina Alex Malanga akiongoza kikao kazi

Kuhusu kufunga mtandao wa inteneti kwenye maeneo ya wazi, Mhandisi Mwasalyanda amesema tayari wamefunga katika maeneo 7 ambayo ni Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Lungemba (Mafinga), Nyerere Square (Dodoma), Ndaki ya Habari na Elimu Angavu (CIVE) Chuo Kikuu cha Dodoma, Soko la Tabora (Tabora), Kiembe Samaki (Unguja) na Soko la Buhongwa (Mwanza). 

"Tumefunga pia katika maeneo mengine 17 katika Viwanja vya Maonyesho ya Sabasaba, lango letu likiwa ni kuongeza wigo wa matumizi ya intaneti, katika mradi huu tumetumia shilingi milionin 374," amesema Mkurugenzi Mkuu wa UCSAF.

Amesema katika kuongeza matumizi ya TEHAMA kwa wananchi, Serikali imewezesha ujenzi wa vituo 11 vya TEHAMA Zanzibar ambavyo ni Tungu wWilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, Mwera Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Mjini Magharibi, Kitongani Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja, Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa kaskazini Unguja na Kiembe Samaki Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi.

Vituo vingine vimejengwa  Mahonda, Kaskazini B Mkoa wa Kaskazini Unguja, Wete Wilaya ya Wetu Kaskazini Pembe, Machomane Wilaya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, Micheweni Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, Jonza Wilaya ya Mkaoni Mkoa wa Kusini Pemba na Bwefumu Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bakari Kimwanga, akitoa neno la shukrani, akimwakiliza Mwenyekiti Deodatus Balile

Amesema wametoa mafunzo ya TEHAMA kupitia vyio vya DIT, UDOM na MUST kwa walimu 3,798 katika shule 1,791, wakati Zanzibar walimu waliopata mafunzo ni 326 na Tanzania Bara 3,180.

"Lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo walimu kutatua matatizo ya vifaa TEHAMA, ambapo katika kipindi cha miaka minne ya Awamu ya Sita walimu 1,585 walipata mafunzo ya TEHAMA." 

Amesema katika jitahada zao za kuhakikisha wanafunzi wanapata mafunzo ya TEHAMA kwa shule za umma, hadi sasa zilizonufaika na mpango huo ni shule 1,121 zilizofikishiwa vifaa ambapo shule hupata kompyuta 5, printa moja na projecta moja, vyote vikigharimu shilingi bilioni 5.94.

Mhariri wa Taifa Tanzania, Hafidh Kido akiuliza swali

"Katika kipindi cha miaka minne ya Awamu ya Sita shule 469 zimepelekewa vifaa vya TEHAMA, lengo ni kukuza ujuzi wa TEHAMA kwa wanafunzi na walimu nchini."

Amesema katika maadhimisho ya siku wasichana yanayofanyika Aprili kila mwakaikiwa na lengo ni kuhamasisha na kukuza uelewa wa masuala ya TEHAMA kwa wasichana, hadi kufikia sasa wametoa mafunzo kwa wanafunzi takribani 1,202.

Ameongeza kuwa, Awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu imetoa mafunzo kwa wanafunzi takribani 490 kutoka shule 304, ambapo mwaka 2024/2025, yalifanyika Aprili kwa wanafunzi kike 248, ambayo yamesaidia kuhamasisha watoto wa kike kupenda masomo ya sayansi.

"Vifaa vya TEHAMA kwa shule zenye watoto wenye mahitaji maalum tumevifikisha katika shule 22, ambavyo ni TV, Braille Machine (Nukta Nundu) Orbit reader (Machine za Kisasa), Laptops, Embosser (Printa ya nukta nundu), Digital voice recorders, Magnifiers, vyote vikitumia ruzuku ya shilingi bilioni 1.8."

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi Peter Mwasalyanda (katikati), Albert Richard (kushoto na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)

Ameongeza kuwa, watapeleka vifaa vya TEHAMA kwa shule zenye watoto wenye mahitaji maalum ambapo mwaka 2024/25, jumla ya vyuo 10 vinatarajiwa kunufaika na mradi huu.

Amevitaja vifaa hivyo ni Braille Display (Nukta Nundu), Embossers (Printa yanukta nundu), Desktop Computer na monitor zake, Laptop, Accessible printer, Projector, Audio player and recorder, Paper shredder, Internet router, Internet Access Point, External hard disk, Flash disk, White Smart board, White board, Colored Printer (Multifunction Printer) na Photocopy Machine ambavyo vimegharimu 700,000,000.

Amesema Vyuo vitakazonufaika ni Sabasaba Vocational and Rehabilitation Centre (Singida Region), Yombo Vocational and Rehabilitation Centre (Dar Es Salaam Region), Luanzari Vocational and Rehabilitation Centre (Tabora Region), Masiwani Vocational and Rehabilitation Centre (Tanga Region), Mirongo Vocational and Rehabilitation Centre (Mwanza Region), Mtapika Vocational and Rehabilitation Centre (Mtwara Region), Kabanga Teachers’ college (KigomaRegion), Mbinga FDC (Ruvuma Region), The Open University of Tanzania na CHAVITA (Temeke Branch).

"Miradi ya kuboresha usikivu wa Redio ya Taifa TBC nchini,  UCSAF inashirikiana na TBC kuboresha usikivu wa matangazo yake, ambapo vituo 19 vitajengwa kwa ruzuku ya shilingi 6,273,974,625."

Ameongeza kuwa, Serikali inatambua umuhimu wa Shirika la Posta nchini na hivyo katika kipindi cha miaka minne Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote imekuwa ikiliwezesha shirika hilo kwa kulipatia vifaa vya TEHAMA ili liweze kutoa huduma kidigitali.

Wahariri na waandishi wa habari wakiwa makini kusikiliza

Amesema Julai 12, 2024, UCSAF ilinunua PDA 250 na kuwakabidhi Shirika la Posta, ambapo gharama za utekelezaji wa mradi huo ni shilingi 161,926,471, huku ikiboresha ofisi ya Msemaji Wa Serikali kwa kununua vifaa vya kisasa vyenye thamani ya shilingi 200,000,000. Lengo likiwa kuongeza ufanisi katika utoaji wa habari.

Wahariri wakifuatuilia wasilisho
Wahariri wakijadiliana jambo wakati wa kikao kazi
Wahariri wakiteta jambo wakati wa kikao kazi

No comments