Header Ads

ad

Breaking News

PUMA Ernergy Tanzania kupitia up ya Mpango makati wa biashara




Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah


 WAWEKEZAJI wa PUMA Energy Tanzania, ambao ni Serikali yaTanzania na Puma Investments Limited, wamekubaliana kufanya mapitio ya mpango mkakati wa biashara wa kampuni hiyo ndani ya mwaka huu. 

 

Mpango huu mpya wa biashara unalenga kuongeza uwekezaji, kupanua mtandao wa usambazaji, na kuongeza idadi ya bidhaa, kwa lengo la kuimarisha mchango wa wa kampunihiyo katika uchumi wa Tanzania, na kukuza maendeleo ya sekta ya nishati.

 

 

Hayo yalibainishwa Jumatatu, Mei 26, 2025 wakati wa ziara ya viongozi wa ngazi ya juu waPUMA Energy kwenye Ofisi ya Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam, wakiongozwa na Bw. Mark Russel, Afisa Mtendaji Mkuu wa PUMA Energy Duniani.

 

Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, alisema mapitio ya mpango mkakati wa biashara yanalenga kuona ukuaji wa kampuni unalinganana vipaumbele vya maendeleo ya taifa, pamoja na kufungua milango ya fursa mpya katika sekta ya nishati.

 

“Uongozi wa kampuni na bodi lazima waangalie upya mpango mkakati wa biashara ndani yamwaka huu ili kuanzia mwaka ujao tuweze kuzitumia vizuri fursa tulizonazo,” alisema Bw.Mchechu, huku akiweka wazi kuwa utekelezaji wampango mkakati mpya utaanza Januari mwakani. 

 

PUMA Energy Tanzania ni kampuni inayomilikiwa kwa asilimia 50 na Serikali ya Tanzania na asilimia 50 na Puma Investments Limited. 

 

Kampuni hii ni tawi la Puma Energy Holdings PteLtd, sehemu ya Trafigura PE Holding Ltd.

 

Bw. Mchechu alisisitiza kuwa uwekezaji wa Serikali katika PUMA ni mkakati muhimuunaolenga kuiwezesha Serikali kuwa  a ushawishi mkubwa katika sekta ya nishati na mtandao wa usambazaji wa mafuta nchini.

 

Kwa upande wake Bw.Russel, alisema Tanzania ina fursa nyingi za kukuza biashara, ikiwemo miradi ya gesi ya asilia (LNG) na gesi ya kupikia(LPG).

 

“Tuna mpango wa kupanua huduma na kuongezaaina za bidhaa tunazotoa kwa jamii. Kupitia ushirikiano wetu na Serikali, tutashirikiana kufungua fursa zaidi na kukuza biashara hii,” alisema Bw. Russel.

 

Bw. Ben Quattara, Mkuu wa kampuni za PUMA Energy Afrika, alibainisha kuwa Tanzania ni mshirika muhimu katika biashara za PUMA barani Afrika na kampuni ina nia ya kuendeleza uwekezaji na faida zaidi hapa nchini.

 

Bi. Fatma Abdallah, Mkurugenzi Mtendaji wa PUMA Energy Tanzania, aliripoti ongezeko la asilimia 51 la faida mwaka 2024 na kufungua vituo vipya vya gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) pamoja na upanuzi wa biashara ya gesi yakupikia (LPG) katika mikoa kadhaa ikiwemo Dodoma, Mwanza, na Arusha.

 

“Tegemeeni mambo makubwa kutoka PUMA Tanzania katika miezi na miaka ijayo,” alimalizia Bi.Abdallah.


 





No comments