Tuesday, June 6, 2017

KIKOSI CHA TAIFA CHA ENGLAND CHANOLEWA MAZOEZI YA KIJESHI

Livermore akibadilishana mawazo na Ryan Bertrand katika kambo ya Royal Marines.

Wachezaji wa timu ya taifa ya England wakiwa na kocha wao, Gareth Southgate wamepelekwa jeshini na kupata mazoezi ya kijeshi ambayo yanaweza kuwajenga kuwa majasiri wakati wakiipigania nchi yao. England wakati ikijiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Scotland, baadaye watashuka uwanjani kupepetana na  kikosi cha Ufaransa.

Wachezaji waliopo jeshini wakijifua kwa ajili ya mchezo na timu zao kwenye mabano ni Jack Butland (Stoke City), Fraser Forster (Southampton), Joe Hart (Manchester City), Tom Heaton (Burnley), wote makipa.

Kwa upande wa mabeki ni Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Aaron Cresswell (West Ham United), Ben Gibson (Middlesbrough), Phil Jones (Manchester United), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Manchester City), Kieran Trippier (Tottenham Hotspur) na Kyle Walker (Tottenham Hotspur) 

Nafasi ya viungo waliojumuishwa kwenye kikosi hicho ni Dele Alli (Tottenham Hotspur), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Adam Lallana (Liverpool), Jesse Lingard (Manchester United), Jake Livermore (West Bromwich Albion), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), na Raheem Sterling (Manchester City).

Kwa upande wa wafumania nyavu ni Jermain Defoe (Sunderland), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Marcus Rashford (Manchester United), Jamie Vardy (Leicester City)

Wachezaji wa kikosi cha Taifa England wakiwa kwenye mavazi ya kijeshi, Adam Lallana, Kyle Walker, Jermain Defoe, Jake Livermore na John Stones
Raheem Sterling na Dele Alli
Aaron Cresswell, Livermore na Defoe wakiwa wametulia
Winga wa tim,u ya taifa ya England na Manchester City, Raheem Sterling akipewa mazoezi.
Kipa wa Southampton, Fraser Forster akizamishwa majini wakati wa mazoezi
Gareth Southgate akizamishwa kwenye maji wakati wa mazoezi ya kijeshi 
Joe Hart na Harry Kane, miongoni mwa wachezaji wanaomsikiliza kamanda wa kikosi cha maji England.

No comments:

Post a Comment