Header Ads

ad

Breaking News

UCHAGUZI YANGA UPIGAJI KURA WAELEKEA UKINGONI, SIMBA AMESHAPIGWA MOJA TAIFA


Zoezi la uchaguzi wa Yanga, lipo katika hatua za mwishoni za upigaji wa kura, baada ya Yussuf Mehoob Manji kukamilisha zoezi la wagombea kujieleza katika kuomba kura kwa wanachama, ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. 
 
Hadi sasa upepo unaonyesha ‘Jeshi la Miamvuli’ litapeta. Yussuf Manji (Mwenyekiti), Clement Sanga (Makamu Mwenyekiti) na Wajumbe Mussa Katabaro, Lameck Nyambaya, Abdallah Bin Kleb na George Manyama.
 
BIN ZUBEIRY ameondoka Diamond Jubilee, na sasa yupo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambako Simba inacheza na URA na mpira umeanza. Lakini anaendelea kuwasiliana na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga juu ya matokeo. Hadi sasa Simba amekwishafungwa 1-0, Owen Kasuule dakika ya 11. Habari na picha kwa hisani ya Bin Zubeiry, www.bongostaz.blogspot.com
Nyambaya kulia, Manji katikati na sanga kushoto

Aaron Nyanda mgombea Ujumbe

Kamati ya Uchaguzi kazini

Mzee Akilimali akipiga kura

Isaac Chanji

Kifukwe na Mosha wakipiga kura

Mzee Jabir Katundu akipiga kura

Katundu anapiga kura

Akilimali anapiga kura

Wazee wanachukua karatasi za kura

Manji na Sanga

Jeshi la Miamvuli linakubalika kwa kila mtu, cheki jembe hapa anatoa peace

Jembe linapigwa muhuri baada ya kura lisije likafanya ujanja ujanja likarudia

Mzee Chabanga Hassan Dyamwale akimpiga muhuri mwanachama baada ya kupiga kura

Jeshi la Miamvuli; Katabaro, Bin Kleb na Manyama

Eric James Shigongo kumbe naye Yanga, siri imefichuka leo

Edgar Fongo kulia akiwa na Lawrence Mwalusako

No comments