Mugisha Nadege kuiwakilisha Burundi Miss East Africa
Mrembo atakayeiwakilisha Nchi ya Burundi katika mashindano ya Miss East Africa mwaka huu amepatikana.
Mrembo huyo wa jijini Bujumbura
anaitwa Miss Mugisha Nadege (21) ana urefu wa futi 5.71 ni mwanafunzi
wa mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha Burundi ambapo anasomea degree ya
mawasiliano.
Mrembo huyo alitangazwa rasmi jana na mratibu wa mashindano ya Miss east Africa kwa Nchi ya Burundi
ambae ni barozi wa amani Nchini Burundi Serge Nkurunziza ambaye
alimtangaza baada ya mrembo huyo kuwashinda warembo wenzake
waliojitokeza kutaka kushiriki mashindano hayo.
Fainali
za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 mwezi
September mwaka huu jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za
Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea,
Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na
Mauritius.
Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam
No comments