Morogoro Bingwa Copa Coca Cola 2012
TIMU ya soka ya Mkoa wa Morogoro jana ilitwaa ubingwa wa Copa Coca Cola, baada ya kuilaza Mwanza bao 1-0, katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Kambukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam, leo.
Washindi walipata bao pekee kipindi cha kwanza
lililofungwa na Salum Ramadhan kwa shuti kali lililokwenda moja kwa moja
wavuni.
Katika mchezo huo, timu zote zilikuwa
zikishambuliana kwa zamu, lakini makipa wa timu zote mbili walikuwa makini
kuhakikisha nyavu zao hazitikiswi.
Bingwa mpya wa michuano hiyo alizawadiwa Morogoro
amekabidhiwa kombe na hundi y ash. milioni nane, wakati mshindi wa pili Mwanza
wakizawadiwa sh. milioni 4.8.
Temeke ambao walishinda nafasi ya tatu walipewa sh.
milioni 3.2, zawadi zote hizo zimetoka kwa waandaaji wa mashindano hayo kampuni
ya Coca Coca Cola nchini.
Mara baada ya mchezo huo kumalizika, Kocha wa
Morogoro, Mecky Mexime, alisema kuwa, hakutegemea vijana wake kama wangeweza
kuibuka na ushindi katika mchezo huo.
“Mchezo ulikuwa mkali na mgumu, sikutegemea kama
vijana wangu wangeweza kuibuka na ushindi, nashukuru wametimiza ndoto zetu,”
alisema.
No comments