Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Ashura Katunzi akitoa wasilisho wakati wa kikao kazi na wahariri na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Septemba 18,2025.
Na Frank Balile
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), katika kipindi cha awamu ya sita kimepata mafanikio makubwa katika utekelezaji wa majukumu yake.
Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt.Ashura Katunzi, ameyasma hayo Septemba 18,2025, alipokutana na wahariri na waandishi wa habari katika kikao kazi jijini Dar es Salaam, ambapo aliyateja mafanikio yao ni amoja na kuimarisha mikakati yake mbalimbali ya kuboresha huduma na kuwezesha biashara, kwa kuinua uchumi wa viwanda, ili vizalishe bidhaa zenye ubora na salama utakaokidhi soko la ndani na nje ya nchi.
Katika kikao kazi hicho kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Dkt.Katunzi, amesema TBS, itajenga maabara katika mikoa ya Mwanza na Dodoma, ambao utagharimu Shilingi 36,802,360,422.39.
Amesema maabara inayojengwa mkoani Dodoma itagharimu Shilingi 24, 723,478,765.48, wakati a Mwanza itatumia Shilingi 12,078,881, 656.91.
Mkurugenzi Mkuu huyo amesema maabara inayojengwa mkoani Dodoma itahudumia mikoa mitatu ya kanda ya Kati ambayo ni Dodoma, Singida na Tabora, Pamoja na mikoa iliyo karibu, wakati ya Kanda ya Ziwa itahudumia mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Geita, Shinyanga na Simiyu."TBS tumetumia Shilingi bilioni 9.8 kwa ajili ya kuimatisha ofisi tisa za kanda zilizopo kwenye mikoa ya Mwanza, Arusha, Mtwara, Mbeya, Dodoma, Kigoma, Pwani, Geita na Dar es Salaam," amesema Mkurugenzi Mkuu wa TBS.
Ameongeza kuwa, mbali na ofisi hizo, wameziimarisha ofisi a mipakani za Tunduma, Kasumulu, Horohoro, Holili, Tarakea, Namanga, Bandari ya Mwanza, Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Kabanga, Rusumo na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro.
Nyingini ni Mutukura, Kasesya, Bandari ya Bagamoyo, Sirari, Bandari ya Mbweni, Bandari ya Dar es Salaam, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam na Bandari ya Tanga.
Afisa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina, Alex Malanga, akitoa mwongozo wakati wa kikao kazi cha Shirika la Viwango Tanzania (TBS), wahariri na waandishi wa habari kilichofanyika Septemba 18,2025 jijini Dar es Salaam"Kwa kuongeza ofisi mpya za kanda, wafanyakazi na vitendea kazi kwa ajili ya kutoa huduma kwa wakati, kumechangia kuimarisha zoezi la ukaguzi wa mara kwa mara katika soko ili kupunguza kwa wakati na kuimarisha zoezi la ukaguzi wa mara kwa mara katika soko ili kupunguza bidhaa hafifu sokoni na kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa bora na salama,"amesema.
Dkt.Katunzi amesema kuwa, Shirika lina kamati za kitaalam 115 katikas sekta za chakula, kemikali, uhandisi wa mitambo, uhandisi wa umeme, uhandisi wa ujenzi, nguo na ngozi, madini na mitambo ya uchimbaji madini na mazingira.
Amesema kamati hizo hushirikiana na wadau mbalimbali katika mchakato wa kuandaa viwango ikiwemo vyuo vikuu, taasisi za utafiti, wafanyabiashara, wazalishaji, vyama vya walaji, bodi za wataalam, taasisi za udhibiti na watunga sera.
Mkurugenzi Mkuu amesema kuwa, Shirika limefanikiwa kuandaa viwango 2,765 vya sekta mbalimbali kwa kuzingatia mahitaji ya soko ambavyo vitawasaidia wafanyabiashara, wajasiriamali na wato huduma kuzalisha bidhaa zenye kukidhi viwango.
"Tumetoa vyeti na leseni za ubora 3,184 kwa wazalishaji, wakiwemo wajasiriamali wadogo 1,359, serikali kupitia TBS imekuwa ikitenga zaidi ya Shilingi milioni 350 kila mwaka kwa lengo la kuwahudumia wajasiriamali wadogo bila malipo. Leseni hizi zimesaidia wazalishaji kuzalisha bidhaa bora," amesema.Amesema jumla ya bidhaa 8,199 na maeneo 47,886 yalisajiliwa, lengo likiwa ni kuhakiki ubora na usalama wa maeneo hayo ili kuendelea kulinda afya za walaji, huku shirika likiendelea na huduma ya usajili wa bidhaa za chakula na vipodozi
Ameongeza kuwa, TBS inahakiki inahakiki bidhaa mbalimbali zinazoingia nchini kutoka nchi za nje, magari yaliyotumika kabla ya kusafirishwa kuja nchini, ambapo jumla ya shehena za bidhaa 153,159 zilikaguliwa kabla ya kuingia nchini kupitia mfumo wa pre-shipment to conformity (PVoC).
Dkt.Katunzi amesema kuwa, shehena za bidhaa 352,103 zilikaguliwa baada ya kufika nchini kupitia mfumo wa Destination Inspection (DI), wakati magari 203,689 yalikaguliwa.Amesema lengo la ukaguzi wa bidhaa hizo ni kutaka kuiepusha Tanzania kuwa jalala la bidhaa duni, pamoja na kulinda afya, usalama na mazingira ya watumiaji.
"Serikali kupitia TBS imetenga Shilingi milioni 350 kila mwaka kwa ajili ya kuwahudumia wajasiriamali wadogo na wa kati nchini, ili kuwasaidia kuhakikisha bidhaa zao zinapata uthibitisho wa ubora."
“TBS itaendelea kushirikiana na watendaji wa halmashauri kote nchini, ili kuwatambua wajasiriamali wenye bidhaa zilizokidhi viwango lakini wameshindwa kupata uthibitisho wa ubora kutokana na changamoto za kifedha,” amesema Dkt. Katunzi.
Kutokana na utendaji kazi mzuri wa TBS, mwaka 2023 ilipata mafanikio makubwa kwa kushinda tuzo ya kuwa mdhibiti bora barani Afrika, ikionesha dhamira ya utendaji bora na chango wake katika kukuza viwango a kudhibiti ubora.
Dkt.Katunzi, amesema TBS imekuwa taasisi ya kwanza kwa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kupata ithibati ya mifumo ya udhibiti ubora bidhaa ya kimataifa katika wigo mpana ndani ya kmuda mfupi, pia ni taasisi ya tatu kupata ithibati iliyotolewa na SADCAS Septemba 2024, hivyo kufanya mifumo hiyo kutambulika kimataifa.
Ameongeza kuwa, mwaka 2025, TBS wamefanikiwa kupata ithibati ya umahiori wa mfumo wa usimamizi wa chakula katika kiwango cha kimataifa cha toleo jipya ISO 22003:2022.
No comments:
Post a Comment