Mlawa awahimiza watanzania kujitokeza kuishangilia Stars
Na Omary Mngindo, Bagamoyo
MDAU wa michezo Aboubakary Mlawa ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo, amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya soka ya Taifa (Taifa Star's) dhidi ya Bukinafaso utaopigwa Jumamosi Agosti 2.Mlawa alisema kuwa mchezo huo wa ufunguzi wa michuano ya AFCON inayowahusu wachezaji wanaocheza ligi za ndani, ni mchezo muhimu kwani utaleta picha nzuri zaidi kwa waTanzania watakapoujaza uwanja.
Alianza kwa kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya kwenye sekta hiyo, ambapo kwa kipindi kifupi nchi imepiga hatua kubwa katika michezo.
"Tunajivunia kuwa na rais anayefuata nyayo za watangulizi wake, ambapo ameitekeleza miradi mingi huku akienda mbele zaidi katika michezo ambapo tunajionea mabadiliko makubwa katika kipindi hiki," alisema Mlawa.
Aliongeza kuwa, katika Uzinduzi wa michuano hiyo inayotaraji kuanza Agosti 2 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Temeke jijini Dar es Salaam ni mchezo muhimu, hivyo kutokana na ukweli huo kuna haja kubwa kwa waTanzania kujitokeza kwa wingi.
Aliwaomba watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia anayoionesha ya kuendeleza kwani maendeleo makubwa yanaonekana kwa timu ya Taifa (Taifa Stars), ambayo katika kipindi hiki imekuwa ikifanya vizuri kwenye michezo mbalimbali.
"Ninaimani kubwa kwamba hamasa inayoendelea kutolewa na viongozi mbalimbali wakiwemo wasemaji wa vilabu vyetu waTanzania wataujaza uwanja kwani wanaimani kubwa na uwezo wa wachezaji wa timu yetu," alimalizia Mlawa.
No comments