DKT.MWINYI ACHUKUA FOMU YA URAIS ZANZIBAR, KIJANI YATAWALA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye pia ni Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo Agosti 30,2025 amechukua fomu ya uteuzi wa kuwania kiti cha Urais wa Zanzibar katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Maisara, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Dkt. Mwinyi ameambatana na Mke wake Mama Mariam Mwinyi pamoja na familia na viongozi mbalimbali wa CCM wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Dkt.Mohamed Said Dimwa pamoja na wanachama na wakereketwa wa maendeleo waliokusanyika kwa wingi kushuhudia hatua hiyo muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar 2025.
Matukio katika picha, hafla ya uchukuaji wa fomu ya uteuzi wa kuwania Kiti cha Urais wa Zanzibar, viwanja vya Mau Ze Dong, leo Agosti 30, 2025.
No comments