NEMC yahamasisha ulaji wa mazao ya bahari
Na Mwandishi Wetu, TangaMKURUGENZI Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), DkT. Immaculate Semesi amewahamasisha watanzania umuhimu wa matumizi ya vyakula vya baharini kwani vinamanufaa makubwa ya afya.
Alitoa ushauri huo jana wakati wa semina iliyoandaliwa na (NEMC) kwa kushirikiana na Taasisi ya West Indian Ocean Marine Science Association ( WIOMSA) jijini Tanga inayojadili kuhusu mchango wa vyakula vya baharini, mitoni na maziwa yaani "Blue foods" katika lishe na usalama wa chakula.
Dk Semesi alisema lengo kuu la semina hiyo ni ni kuhamasisha umuhimu wa vyakula vya baharini, katika mito na maziwa yaani "Blue foods" katika lishe bora kwani vyakula hivyo vinamanufaa makubwa katika Afya ya binadamu.
Alisema ni muhimu wananchi kuzingatia chakula kinachotokana na mazao ya baharini kwani vinajenga afya hivyo ni matarajio kuwa taifa litaendelea kuwa na watu wenye uelewa na kuweza kujitegemea.
Akizungumza katika ufunguzi wa semina hiyo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa buluu na Uvuvi Zanzibar, Zahor Kassim Mohamed, alisema vyakula vya buluu "Blue foods" ni muhimu katika lishe bora na usalama wa chakula.
"Vyakula vya buluu yaani"Blue foods" kama vile samaki, dagaa, kaa, majongoo wa baharini, mwani na viumbe wengine vinamchango mkubwa katika lishe bora, usalama wa chakula, uchumi wa Kaya na ajira,"alilisema Zahor Mohamed.
Akiwasilisha mada kwenye semina hiyo, Mkurugenzi wa Taasisi ya WIOMSA, Dk Arthur Tude, alisema Taasisi hiyo imejikita katika tafiti za kuboresha lishe bora na kuelimisha jamii kuhusu vyakula vya baharini.
Alisema taasisi imeamua kushirikiana na NEMC Pamoja na Taasisi nyingine kuhamasisha jamii kuhusu uvunaji wa vyakula vya baharini vyenye lishe bora.
Aidha, Zahor alisisitiza kuwa ni muhimu Sekta zote binafsi na za Serikali, Taasisi na washirika wa maendeleo na jamii za uvuvi kuhakikisha kuwa "blue food" zinachangia kwa ufanisi kutokomeza njaa, kuongeza kipato na kulinda Mazingira ya bahari, mito na maziwa ambavyo ni rasilimali muhimu za kufuga vyakula buluu.
Aliongeza kuwa, licha ya changamoto zinazokabili ustawi wa vyakula vya buluu, Serikali imeweza kuimarisha Sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kuwezesha ufugaji samaki katika mabwawa ya kisasa.
Alisema serikali imewezesha vikundi vya wanawake na vijana katika mnyororo wa thamani wa mazao ya maji, kushiriki katika juhudi za kimataifa za na kikanda kama vile Blue Economy na mabadiliko ya mifumo ya chakula duniani.

No comments