Makalla: Awamu ya pili mradi wa maji Mwanga, Same, Korogwe kutekelezwa
Katibu wa NEC, Itikadi Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla kizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Same mkoani Kilimanjaro, jana Jumatano Juni 11,2025
Na Mwandishi Wetu, Same Magharibi
Na Mwandishi Wetu, Same Magharibi
KATIBU wa NEC, Itikadi Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema awamu ya pili ya mradi wa maji wa Same - Korogwe utaanza Hedaru kuelekea Korogwe.
Pia, amempongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha kutolewa kwa fedha kiasi cha Sh bilioni 400 ili kukwamua mradi wa maji ambao ulikwama kwa muda mrefu.
Makalla ameeleza hayo Juni 11,2025 wakati akizungumza na wananchi wa katika eneo la Hedaru Jimbo la Same Magharibi wilayani Same mkoani Kilimanjaro akihitimisha ziara yeke katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Makalla amesema awamu ya pili ya mradi huo utapita katika vijiji 24 kutokea Same Mjini kupita Hedaru na vijiji Vitano vya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.
Awali, Makalla amesema mradi huo wa maji uliwasumbua kwa muda mrefu kwa awamu mbili za uongozi zilizopita lakini chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia matokeo yameonekana kwa kuidhinisha kutolewa kiasi tajwa cha fedha kukwamua mradi huo.
Makalla amesema mradi wa Mwanga -Same hadi Korogwe ulipata mkandarasi na akawa anasua sua katika utekelezaji akafukuzwa na hadi hapo umetumia jumla ya Sh. bilioni 400 katika utekelezaji wake na maji yamefika Same Mjini na Mwanga.

No comments