BALOZI NCHIMBI MSIBANI KWA MZEE MONGELLA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akisaini kitabu cha maombolezo na kumpatia pole, Mama Gertrude Ibengwe Mongella, familia yake na waombolezaji wengine, kwa msiba wa Mzee Silvin Ibengwe Emmanuel Mongella, ambaye ni mwenza wa Mama Mongella, leo Jumanne, Juni 3,2025, eneo la Makongo juu, jijini Dar es Salaam.
Marehemu Mzee Mongella (85), ambaye pia ni baba mzazi wa John Mongella, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (bara), alifariki Mei 31,2025, na mazishi yake yamepangwa kufanyika huko Mwanza, Juni 7 2025.
No comments