Header Ads

ad

Breaking News

RAIS MWINYI KUELEKEA UINGEREZA KUSHIRIKI MKUTANO WA CTIS

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dkt.Hussein Ali Mwinyi alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mbelwa Kairuki katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow jijini London

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dkt.Hussein Ali Mwinyi aliondoka nchini kuelekea jijini London, nchini Uingereza kwa ziara ya kikazi kuanzia Aprili 6 hadi 9, 2025 kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa Biashara na Uwekezaji wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Trade & Investment Summit 2025).

Katika ziara hiyo Rais Dkt.Mwinyi matukio mengine atakayoshiriki ni kukutana na viongozi waandamizi wa Serikali ya Uingereza na taasisi zake, atakutana na Diaspora wa Tanzania waliopo nchini Uingereza, atakutana na Sir Tony Blair, Waziri Mkuu mstaafu na Kiongozi wa Tony Blair Institute (TBI), pia atakutana na wadau wa uwekezaji katika uchumi wa bluu.

Rais Dkt.Mwinyi atakutana na wadau wa uwekezaji katika sekta ya utalii, filamu, viwanda, nishati ikiwemo pia mafuta na gesi.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi atashuhudia kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano baina ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Chuo Kikuu cha Kent kwa ajili ya utafiti wa kilimo cha Mwani pamoja na MOU kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Kampuni ya Perry Engineering ya Uingereza kuhusu usambazaji wa mbegu za mwani.


No comments