Dkt.Mwinyi ateta na jopo la Majaji Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kulia)
Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Majaji Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika(SEACJF), unaotarajiwa kufanyika Zanzibar mwakani ni fursa muhimu ya kuimarisha ushirikiano na kuimarisha utendaji wa mahakama kwa nchi hizo.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na jopo la Majaji Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika waliofika Ikulu kuonana naye.Amefahamisha kuwa, mbali na kuwaleta pamoja mkutano huo itasaidia kubadilishana uzoefu baina ya nchi na nchi na kujadili kwa pamoja changamoto za kiutendaji wa mahakama kwa nchi wanachama.
Aidha, amewahakikishia majaji hao kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha mkutano huo wa kwanza kufanyika nchini.
Amewasisitiza majaji hao wakati wa mkutano huo kuvitembelea vivutio vya utalii vya Zanzibar na hatimaye kuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Zanzibar katika nchi zao hatua itayochochea kukuza sekta ya utalii inayochangia asilimia asilimia 30 ya pato la Taifa.
Naye, Rais wa Jumuiya hiyo Jaji Mkuu wa Eswatini Moses Cuthbert Maphalala amesema lengo kuu la mkutano huo ni kulinda na kuimarisha utawala wa sheria, uhuru wa mahakama, kubadilishana uzoefu pamoja na kuhakikisha mihimili ya nchi inafanya kazi kwa pamoja.
No comments