Header Ads

ad

Breaking News

Wanafunzi wa zamani Sekondari Lugoba waitwa

Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne Sekondari ya Lugoba, iliyopo Kitongoji cha Lunga Kata ya Lugoba Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Picha na Omary Mngindo

Na Omary Mngindo, Lugoba

WATANZANIA waliosoma shule ya Sekondari ya Lugoba iliyopo Kata ya Lugoba, halmashauri ya Chalinze, Bagamoyo Pwani, wameitwa kusaidia maendeleo ya shule hiyo.

Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na mmoja wa wajumbe wa Bodi ya shule John Chiwaligo, kwenye Maafali ya 33 akisema kuwa ni vema kwa waTanzania waliosoma hapo wawe nchini au nje kufika kusaidia kupunguza changamoto.

Alisema kuwa mbali ya Serikali Kuu na Halmashauri, mdau mmoja tu Subhash Patel (Marehemu) ndio alikuwa akijitoa wakati wa uhai wake, kujenga na kukarabati miundombinu ya shule ikiwemo ukumbi unaotumika kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi pia mikutano.

"Hapa tulipokaa ni juhudi za mtu mmoja aliyetolea fedha zake kuita mafundi kujenga jengo ili, nitoe wito kwa vijana waliosoma hapa kokote walipo duniani ebu warudi kurudisha fadhila, wenzenu tuliopo hapa tunahitaji misaada yenu," alisema Chiwaligo.

Taarifa ya Mwalimu Mkuu wa shule Alhaj Abdallah Sakasa imeelezea mafanikio yaliyopatikana kupitia ushirikiano wa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na aliyekuwa rafiki yake mkubwa wakati wa uhai wake Mzee Subhaah Patel ambao waliisaidia kufikia ilipo sasa.

"Sisi jamii ya Lugoba tunatoa shukrani nyingi kwa mzee wetu Dkt. Jakaya Kikwete yeye binafsi na aliyekuwa rafiki yake mkubwa Mzee Subhash Patel, kwa misaada mikubwa waliyoipatia shule kwani bila wao isingekuwa hivi ilivyo," ilieleza sehemu ya taarifa yake.

Sanjali na hayo "Tunaishukuru Serikali chini ya rais Dkt. Samia Suluhu kwa kutuletea fedha za ujenzi wa vyoo matundu 20, pia tunaomba kadri fedha zitakapopatikana tusaidiwe ili tujenge mabweni mawili, moja la wasichana na lingine wavulana,".

Ikizungumzia jitihada za shule kupambana na changamoto hiyo, taarifa ya Sakasa imeeleza kuwa wamefyatua tofali za kuchota 35,000, kazi iliyofanywa na wanafunzi hao.

Zacharia Weibuna Afisa Elimu, Vifaa na Taaluma Sekondari akimwakisha Afisa Elimu Sekondari aliwashukuru na kuwapongeza wazazi nawalezi kwa ushirikiano wanaoupatia uongozi wa shule chini ya Mwalimu Mkuu Sakasa.

"Kwaniaba ya Afisa Elimu Sekondari tunawapongeza walimu kwa kazi kubwa na ngumu mnayoendelea kuitekeleza, kuhusu upungufu wa walimu, halmashauri tutaitazama shule kwa jicho la kipekee," alisema Weibuna.

Mohamed Mzimba aliwaomba wazazi na walezi kwa kipindi hiki kila mmoja kwa dini yake kuwaombea watoto hao waweze kufanya vizuri katika mitihani yao ya kumaliza elimu hiyo ya kidato cha nne.

Diwani wa Kata ya Lugoba Rehema Mwene alielezea imani yake kwa niaba ya wazazi wote, juu ha uwezo wa wanafunzi hao kufanya vizuri katika mitihani inayowakabili, ya kuingia kidato cha tano.

Taarifa ya wahitimu hao iliyosomwa na Harafa Sakasa imeelezea changamoto ya kukosekana kwa vifaa vya Maabara shuleni hapo hususani vya maaomo ya sayansi, kufuatia uwepo wa idadi kubwa ya wanafunzi.

No comments