Header Ads

ad

Breaking News

Goba Hills Marathon


KLABU ya wakimbia kwa miguu wa Goba Hills Marathon imetangaza marathoni ya msimu wa sita itakayofanyika February Mosi 2025 Jijini Dar es salaam ikiwa na lengo la kukusanya kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia afya ya ustawi kwa shule za msingi na sekondari.

Mbio hizo zinazotarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya washiriki 2,000 zitajumuisha watu wote kuanzia umri wa miaka minne zikikimbiwa umbali wa kuanzia kilomita 5,10,21 na 42.

Kwa niaba ya wadhamini wa mbio hizo taasisi ya Chatsoko, Afisa Mauzo Christine Abulitsa amesema miongoni mwa faida katika ni kurahisisha usajili pamoja na kufanya malipo ya haraka kwa washiriki wa mbio hizo.

Goba Hills Marathon, ni msimu wake wa sita tangu kuanzishwa kwake, ikiwa na lengo la kukusanya kiasi cha shilingi milioni 100. 





No comments