Dkt. JKCI kupewa tuzo kutoka American College of Cardiology - ACC
Na Mwandishi Maalumu
CHUO cha taaluma ya magonjwa ya moyo (American College of Cardiology – ACC) cha nchini Marekani kutoa tuzo kwa daktari bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Khuzeima Khanbhai.
Tuzo hiyo inatolewa baada ya kamati ya tuzo ya ACC kupokea fursa za wanazuoni za Hani Najm Global ambao huwapa washindi fursa kubadilishana ujuzi na wataalamu wenzao yatakayofanyika katika kliniki ya Clevaland iliyopo Ohio’s.
Akizungumzia tuzo hiyo Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Khuzeima Khanbhai alisema mbali na kupewa tuzo hiyo wakati wa mkutano wa ACC utakaofanyika Chicago mwezi Machi mwakani pia atapata fursa ya kushiriki mafunzo ya wiki nne yatakayotolewa katika kliniki ya Clevaland iliyopo Ohio’s nchini Marekani.
“Fursa hii hutolewa kila mwaka kwa wataalamu wa magonjwa ya moyo duniani ambapo mwaka huu tumepata nafasi wataalamu watatu nikiwemo mimi kutoka nchini Tanzania," alisema Dkt. Khuzeima
Dkt. Khuzeima alitoa shukrani zake kwa Chuo cha taaluma ya magonjwa ya moyo (American College of Cardiology – ACC) kwa kumpa nafasi hiyo ambayo inaenda kumuongezea utaalamu zaidi katika kutoa huduma kwa wagonjwa wa moyo.
No comments