Header Ads

ad

Breaking News

Mfuko wa Taifa wa Maji watekeleza agizo la Dkt.Samia

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF), Wakili Haji Nandule akitoa wasilisho wakati wa kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali na waandishi wa habari chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina leo Oktoba 31,2024 jijini Dar es Salaam


Na Mwandishi Wetu

MFUKO wa Taifa wa Maji (NWF), umefanikisha ujenzi wa  miradi ya maji kwa vitendo katika maeneo mbalimbali yenye uhitaji mkubwa.

Mafanikio hayo ni utekelezaji wa maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani kupitia miradi mbalimbali ya maji inayoitekelezwa kote nchini.

NWF yenye jukumu la kutafuta fedha za utekelezaji wa miradi ya maji mjini na vijijini, huku serikali ya awamu ya sita ikihakikisha kazi hiyo inafanikiwa na wananchi wanafikiwa na huduma ya maji safi na salama.

Akizungumza katika kikao kazi kati ya NWF, wahariri na waandishi wa habari, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF), Wakili Haji Nandule, anasema mfko huo ulianzishwa mwaka 2015/2016 chini ya Sheria ya Usambazaji Majisafi na Usafi wa Mazingira namba 5 ya Mwaka 2019.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF), Mhandisi Abdallah Mkufunzi akifafanua jambo katika kikao kazi

Anasema hiyo ni taasisi ya fedha yenye lengo la kutoa fedha za utekelezaji miradi ya usambazaji majisafi kwenye maeneo yenye uhaba na utunzaji vyanzo vya maji nchini.

Wakili Nandule anasema lengo la kuanzishwa mfuko huo ni kuiwezesha serikali kuwa na chanzo cha uhakika na endelevu cha fedha ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maji.

Anasema NWF inajivunia mafanikio makubwa ya utekelezaji wa majukumu yake katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt.Samia tangu aingie madarakani.

kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vinavyoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kupitia taasisi na mashirika yaliyo chini ya ofisi hiyo kuelezea majukumu yao na mafanikio katika miradi wanayoitekeleza.

 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Umma na Mawasiliano Ofisi ya Hazina, Sabato Kosuri akieleza jambo wakati wa kikao kazi cha Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF), wahariri na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2024 jijini Dar es Salaam

Kuanzia Julai, 2021 hadi Juni, 2024, NWF imetoa fedha za kutekeleza miradi ya maji 998, kati ya hiyo, miradi 354 imekamilika na kunufaisha wananchi milioni 5.3.

Anasema serikali ya Awamu ya Sita inafanya kazi kubwa ya kutekeleza miradi ya maji kwa vitendo, hivyo watahakikisha fedha wanazopokea ili kutekeleza miradi hiyo zitatumika kama ilivyokusudiwa , lengo likiwa ni kuboresha huduma za maji nchini.

Anaongeza kuwa, lengo la kuanzishwa mfuko huo ni uwezeshaji wa fedha za kutekeleza miradi ya usambazaji majisafi katika maeneo yenye uhaba na kutunza vyanzo vya maji.

Anasema katika kipindi hicho hadi kufikia Julai, 2024, shilingi bilioni 5.3 zimetolewa kama mkopo katika Mamlaka za Maji ili kutekeleza miradi mbalimbali.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile akitoa neno la shukrani

Kwa upande wa mafanikio ya mfuko huo, Mtendaji mkuu wa Mfuko huo, anasema maafisa 150 kutoka Ofisi za RUWASA, Mamlaka za Maji, Bodi za Maji za Mabonde kwenye mikoa mbalimbali nchini wamepatiwa mafunzo ya kuandaa maandiko ya miradi.

Mikoa iliyopatiwa mafunzo hayo ni Rukwa, Songwe, Iringa, Njombe, Mbeya, Sumbawanga, Shinyanga, Kigoma, Ruvuma na Morogoro.

Kuhusu miradi ya utunzaji rasilimali za maji, miradi 104 ya uhifadhi, uendelezaji vyanzo vya maji imetekelezwa ikijumuisha uhifadhi wa vyanzo vya maji zaidi ya 92.

Anasema kuwa, kuna ujenzi wa bwawa moja, ukarabati wa mabwawa saba, uchimbaji wa visima virefu zaidi ya 50 na kurudisha mito mitano iliyopoteza mikondo yake. 

Wakili Nandule anasema kuwa, wapokeaji fedha za miradi ya mfuko ni Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Mamlaka za Maji, Bodi za Maji za Mabonde.

Pamoja na majukumu hayo, pia Mfuko huo unatoa mikopo yenye masharti nafuu kwa watekelezaji ili wawekeze katika mirafi ya maji.

Maofisa wa Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF) na wahariri wakisikiliza

Pia, wanafuatilia matumizi ya fedha zinazotumwa kwa watekelezaji miradi, kuwajengea uwezo wa miradi ya maji ili waweze kusimamia kwa ufanisi.

Mfuko una jukumu la kumshauri Waziri wa Maji kuhusu miongozo ya utoaji mikopo kwa mamlaka husika, kuandaa miongozo ya kiutendaji kuhusu utoaji mikopo na misaada kwa watekelezaji miradi ya maji nchini.

“Kwa sasa chanzo kikubwa cha fedha kwa mfuko ni tozo ya mafuta sh. 50 kwa kila lita moja ya petrol na dizeli ambayo inatozwa kwa mujibu wa sheria namba 16 ya mwaka 2015,”anasema.

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF), Wakili Haji Nandule akiwasilisha wasilisho la Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF)

                                               Mhariri Bakari Kmwanga akiuliza swali

Mhariri Lilian Timbuka akiuliza swali katika kikao kazi
Mhariri Saed Kubenea akiuliza swali
Wahariri wakifuatilia

Wahariri akiwa makini kusikiliza wasilisho

No comments