TANTRADE WEKENI SEHEMU MAALUM KWA WAANDISHI-BUKUKU
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Latifa Khamis |
Na Mwandishi Wetu
MAHRIRI na mmiliki wa mitandao ya Fullshangwe, John Bukuku, amemshauri Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Latifa Khamis, kuweka utaratibu kwa wanahabari kuwa na sehemu maalumu katika viwanja vya Sabasaba ili waweze kufanya kazi zao kwa uhuru.
Akizungumza kwenye semina fupi iliyoandaliwa na TanTrade chini ya utaratibu wa Ofisi ya Hazina, Bukuku alimweleza mkurugenzi huyo adha wanayopata wanahabari wakati wa kuandika na kuripoti habari za matukio wakati wa Sabasaba.
“Mkurugenzi, wanahabri wanapata tabu sana wakati wa kuripoti na kuandika matukio katika viwanja vya Sabasaba, kwa ujumla wetu tunaomba kuwe na mazingira mazuri ili wanahabari waweze kufanya kazi zao kwa uhuru,” amesema Bukuku.
Mkurugenzi Latifa amekubaliana na Bukuku kwamba, kuna kila sababu ya kuandaa mazingira hayo huku akiahidi kulifanyia kazi suala hilo.
Mhariri na mmiliki wa mtandao wa Fullshangwe, John Bukuku (aliyesimama), akitoa ushauri |
No comments