Header Ads

ad

Breaking News

RAIS SAMIA KUFUNGUA MKUTANO JUKWAA LA MAJAJI WAKUU

TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Mashariki na Kusini mwa Afrika (SEACJF), utakaofunguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Oktoba 24,2023, jijini Arusha.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mkutano huo, ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Ignas Kitus, alipokutana na wahariri Septemba 1, 2023, jijini Dar es Salaam.

Amesema, pamoja na mambo mengine, mkutano huo utajadili namna bora ya utatuzi wa migogoro ya biashara na uwekezaji kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Jaji Kitus amesema, mkutano huo utahusishwa jopo la majaji wakuu kutoka nchi 16 zikiwemo Namibia, Botswana, Kenya, Uganda na Zambia. 

"Mkutano wa Jukwaa la Majaji Wakuu ni Sehemu muhimu ya kukuza ushirikiano, kubadilishana maarifa na maendeleo ya mifumo ya mahakama ya eneo la Kusini mwa Afrika," amesema Jaji Kitus.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile





No comments