Header Ads

ad

Breaking News

CHALAMILA AKUTANA NA KAMATI YA MAANDALIZI MKUTANO MKUU WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Septemba 1,2023 amekutana na Kamati ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Baraza la Michezo ya Majeshi duniani ofisini kwake Ilala Boma jijini Dar es Salaam.

Chalamila akizungumza mbele ya ujumbe huo wa JWTZ, kwanza amemshukuru Mkuu wa Majeshi, John Jacob Mkunda na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan, kutokana na mkutano huo mkubwa wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani kufanyika nchini, hususan Mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema mkutano huo utafungua fursa za kiuchumi kwa watanzania na ni kiashiria cha nguvu ya diplomasia katika kukuza uchumi wa Taifa.

Mkuu wa Mkoa amesema katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia, taifa linashuhudia kuimarika kwa diplomasia ya Uchumi kwa kasi kubwa, ambapo mwezi uliopita Mkutano Mkubwa wa kujadili mtaji wa rasilimali mali watu ulifanyika nchini na kuhudhuriwa na mataifa zaidi ya 40.

Mwezi huu tunatarajia kuwa na Kongamano  kubwa la mifumo ya Chakula Afrika ( AGRF SUMMIT), inayotarajiwa kuanza Septemba 4 hadi 8, 2023 jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa JNICC, hayo yote ni matunda ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kuimarisha diplomasia ndani na nje ya nchi, hivyo mkoa kwa heshima kubwa ya Rais umepokea kwa furaha taarifa ya kufanyika tena kwa kwa mkutano mkubwa wa Baraza la Michezo ya Majeshi duniani.

Chalamila amesema hiyo ni fursa nyingine kwa taifa, si tu kwa upande wa michezo bali pia ni fursa ya kukuza uchumi wa Watanzania, hivyo, Mkoa uko tayari kutoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha mkutano huo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Meja Jenerali Francis Mbindi, amesema mkutano huo unatarajiwa kufanyika mkoani Dar es Salaam kuanzia Mei 12 hadi 19, 2024, ambapo nchi zaidi ya 140 zitashiriki, lakini ufunguzi wake utafanyika Mei 14,2024 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na utafungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan, hivyo wamekutana na mkuu wa Mkoa kwa lengo la Kujitambulisha na kuomba msaada wa hali na mali katika kufanikisha mkutano huo wa kihistoria.







No comments